27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

Mnyeti ‘avalia njuga’ migogoro ya ardhi Kiteto

Mohamed Hamad

Mkuu wa mkoa wa Manyara, Alezander Mnyeti amewataka wananchi wa Wilaya ya Kiteto kuondoa migogoro ya ardhi vichwani mwao na kuruhusu maendeleo mengine kutawala.

Mnyeti ametoa kauli hiyo alipokuwa akihitimisha ziara yake ya siku tano mjini Kibaya

wilayani Kiteto ambapo amesema kuwa wananchi wengi wamekuwa na mtazamo wa migogoro ya ardhi vichwani kila kukicha na kutoyapa nafasi maendeleo mengine na kwamba serikali ya awamu ya tano imejielekeza zaidi katika uchumi wa kati hivyo wananchi wanapaswa kuwa na falsafa hiyo na hasa masuala ya elimu, afya, maji na miundombinu.

Mkuu huyo wa mkoa aliwaelekeza viongozi wa Kiteto kuacha kulalamika na kuhakikisha wanaitatua migogoro ya wakulima na wafugaji sambamba na kuwaelekeza wananchi katika kuyafikia maendeleo hayo.

Akiwa katika vijiji vya Matui, Bwawani, Magungu Orkine na Kibaya aliwarejeshea maeneo baadhi ya wananchi ambao waliporwa na Serikali za vijiji na hata taasisi  zisizo za Kiserikali kwa uonevu.

“Rudini kwenye maeneo yenu halafu nisikie mnasumbuliwa, sitamani kusikia mtu mwenye haki yake anabughudhiwa, wale wenye nyaraka halali leteni hapa nikibaini haki hiyo ni yako nakupa hapa hapa sitaki maneno,” amesema.

Aidha Mnyeti amezindua madarasa, matundu ya vyoo, ofisi za walimu zilizojengwa na serikali kupitia mfuko wa (EP4R) lipa kulingana na matokeo, akisema zimetendewa haki kwani Kiteto inaongoza Kimkoa kwa utekelezaji wa miradi hiyo.

“Mpaka sasa wilaya ya Kiteto inaongoza Kimkoa katika utekelezaji wa miradi hii na mimi nisema tu kuwa ni vyema maeneo mengine kuja kujifunza hapa namna wanavyotekeleza kwani fedha za madarasa matatu zinajenga madarasa manne hili ni jambo jema,”amesema Mnyeti.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles