24.2 C
Dar es Salaam
Monday, March 27, 2023

Contact us: [email protected]

Mnara wa kumbukumbu ya migogoro ya wakulima, wafugaji kujengwa Morogoro

Ashura Kazinja, Morogoro

Mnara utakaotumika kama kumbukumbu ya matukio ya vurugu zilizotokana na migogoro ya wakulima na wafugaji, unatarajiwa kujengwa mkoani Morogoro katika Kijiji cha Kambala wilayani Mvomero.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk. Kebwe Steven amesema hayo leo, katika kongamano linalolenga kuhubiri amani,  na kuongeza kuwa serikali ya mkoa inaona ni wakati mwafaka wa kuweka kumbukumbu ya matukio ya vurugu hizo, zilizosababisha baadhi ya watu kupoteza maisha, mali na wengine kuachwa na ulemavu wa kudumu.

“Uamuzi huo umefikiwa baada ya kuonekana kuisha kabisa kwa migogoro baina ya makundi hayo mawili ambapo tangu mwanzoni mwa mwaka 2016 hakujaripotiwa kutokea kwa mgogoro wowote wa kuhatarisha usalama, huku jamii zote mbili wakiishi kwa kutegemeana baada ya kuwepo kwa mpango wa matumizi bora ya ardhi.

“Hiyo ni sehemu ya kukumbuka ndugu zetu waliopotea katika mgogoro wa wakulima na wafugaji, tujenge mnara kuonyesha kwamba kulikuwa na vita sasa vimekwisha, tutangaze uhuru kwa kushirikiana,” amesema Dk. Kebwe.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Amani Mkoa wa Morogoro, Jacob Ole Mameo amesema kwa sasa amani imetawala tofauti na awali ambapo viongozi walikuwa wakifika katika kijiji hicho walikuwa wanakutana na malalamiko mengi, tofauti na sasa ambapo mambo yamebadilika na kwamba viongozi wanafika kushuhudia au kufungua mambo mazuri yanayoanzishwa na wananchi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,211FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles