24.4 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Mmuya: Tukusanye taarifa za Kijografia kwa kila nyumba tunayoitambua

Na Mwandishi Wetu, Pwani

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, Kaspar Mmuya amekemea tabia ya wachukua taarifa wasio waadilifu wanaochukua taarifa za kijiografia (GPS) za sehemu moja kutolea taarifa kwenye eneo jingine nakwamba jambo hilo linaharibu kazi data na linasababisha mfumo kutoa taarifa zisizosahihi.

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, Kaspar Mmuya akimsikiliza Mwananchi katika Mtaa wa Mkwanyule akijieleza jinsi alivyopokea operesheni ya Anwani za makazi Halmashauri ya wilaya ya Kilwa.

“Watendaji mkagaue na kujiridhisha kuhusu taarifa za kijiografia (GPS), hasa pale inapotokea taarifa hizo kufanana eneo moja na jingine,” amesema Mkuu Mmuya.

Mmuya ameyasema hayo Mei 17, mwaka huu katika ziara yake ya kukagua utekelezaji wa operesheni ya anwani za makazi katika Wilaya ya Kilwa na Rufiji mkoani Pwani nakusisitiza kuwa lazima taafa za kijiografia zikusanywe kwa kila nyumba ambayo inaenda kutambuliwa kwa sababu taarifa hizo zinatofautiana.

“Ninawapongeza wananchi wa Kilwa na Rufiji kwa uelewa na muitikio wao katika kutekeleza Operesheni ya anwani za makazi na umuhimu wake kwa Sensa ya watu na makazi. Tuendelee kuhamasisha wananchi juu ya umuhimu wa operesheni ya anwani za makazi.

“Pia ninatoa wito kwa wananchi wote, kujiwekea namba ya kudumu kwenye mageti au milango ni jukumu lao,” amesema Mmuya.

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, Kaspar Mmuya akizungumza jambo na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji, Juma Ligomba Na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Rufiji, John Kayombo mbele ya ofisi ya Mkuu wa wilaya hiyo wakati akikagua utekelezaji wa operesheni ya Anwani za makazi wilayani humo.

Akihitimisha Injinia wa Wakala wa Barabara za mjini na vijijini (TARURA), Agatha Mtwangambate amesema kwa awamu ya kwanza  idadi ya vibao vya barabara ni kwa ajili ya barabara zote zilizosajiliwa, na vitawekwa katika mwanzo wa barabara na mwisho wa barabara.

“Kadri operesheni ya anuani za makazi inavyoendelea tutaanza kuzitambua barabara mpya na kuziwekea vibao,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles