25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

Mmuya aridhiwahwa na ujenzi wa kituo cha uratibu na udhibiti wa maafa

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Naibu katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu), Kaspar Mmuya ametembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo cha Uratibu na Maafa unaoendelea katika eneo la Ujenzi la Nzuguni B jijini Dodoma unaogharimu zaidi ya Sh bilioni mbili.

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu),Kaspar Mmuya (katikati) akikagua Ramani ya Mradi wa Kituo cha Uratibu na Maafa katika eneo la ujenzi Nzuguni B jijini Dodoma.

Akizungumza mara baada ya kukagua ujenzi huo Naibu Katibu Mkuu, Kaspar Mmuya amesema Ofisi yao  inasimamia ubora wa shughuli, Thamani ya Fedha pamoja na kasi ya ujenzi wa miradi  hivyo licha ya changamoto ndogondogo zilizopo katika mradi huo ni vizuri mkandarasi akaongeza spidi ya ujenzi wa mradi huo.

“Ni vizuri kutumia kipindi ambacho hakina changamoto nyingi kufanya kazi nyingi  kwa uharaka ili changamoto zikija zile ambazo huwezi kuzikabili inakuwa rahisi ambapo umeshafika sehemu ya juu kwa hiyo mimi wito wangu ni kuongeza spidi maana kuongeza spidi ni jambo la kawaida tu ni kuongeza nguvu kazi, kuongeza vifaa, unaongeza muda wa kazi basi,” amesema Mmuya.

Aidha, Mmuya ameahidi kurudi kutembelea mradi huo ndani ya mwezi mmoja na kumtaka Mkadiriaji wa Majengo Sauden Anania kuhakikisha anampa taarifa ili kushirikiana na ofisi yake na kuifanya kazi kuwa rahisi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles