22.6 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 17, 2024

Contact us: [email protected]

Mloganzila yafanikisha upasuaji uvimbe kwenye ubongo

Tunu Nassor-Dar es Salaam

Kwa mara ya kwanza, Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila imefanya upasuaji mkubwa wa kuondoa uvimbe katika mishipa ya damu kwenye ubongo (cerebral aneurysms).

Akizungumza leo Juni 18, wakati wa kutoa ruhusa kwa mgonjwa aliyefanyiwa upasuaji Cosilla Ntambilla, Mkazi wa kurasini , daktari bingwa wa upasuaji wa ubongo na mishipa ya fahamu hospitalini hapo, Dk. Raymond Makundi amesema kufanikiwa kwa upasuaji huo kutapunguza rufaa za wagonjwa kwenda kutibiwa nje ya nchi na matibabu ya ubingwa wa juu yanatolewa nchini.

“Upasuaji huu ambao umechukua saa sita umefanywa na wataalam wa Hospitali ya Taifa Muhimbili – Mloganzila kwa kushirikiana na daktari bingwa mshauri wa upasuaji wa ubongo na mishipa ya fahamu Prof. Huh Seong kutoka Yonsei, Korea Kusini,” amesema Dk. Makundi.

“Kwa mgonjwa kama huyu mmoja ambaye tumemfanyia upasuaji endapo angepelekwa nje ya nchi ingegharimu Sh milioni 21 ikiwa ni gharama ya upasuaji pekee,’’ amesema Dk. Makundi.

 Naye daktari bingwa wa upasuaji wa ubongo na mishipa ya fahamu Dk. Alvin Miranda, amesema lengo la upasuaji ni kufunga vivimbe hivyo kwa kutumia vifaa tiba maalum (aneurysm clips), ili kuzuia damu isiendelee kuvuja katika ubongo.

“Mgonjwa anapopata tatizo la kuvuja damu kwenye ubongo kwa mara ya kwanza anakua katika hatari ya kupoteza maisha kwa asilimia 30, wakati akivuja damu kwa mara ya pili inaweza kusababisha kifo kwa asilimia 70 hadi 80” amesema Dk. Miranda.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles