23.9 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

MLIPUKO WAUWA WATU 29 MEXICO

bbxnt9u-img

Takribani watu 29 wamekufa na wengine zaidi ya 70 kujeruhiwa kutokana na mlipuko mkubwa wa moto uliotokea katika Soko la San Pablito kilomita 36 nje kidogo ya mji wa Mexco.

Taarifa zilizopo kwasasa zinasema kati ya hao majeruhi zaidi ya 70, 20 wamepata nafuu na kuruhusiwa kurudi nyumbani.

Walioshuhudia mlipuko huo wamesema moto ulikuwa mkubwa na kusababisha moshi mzito kutanda hivyo kusababisha taharuki katika eneo hilo la soko na kuwafanya watu kukimbi hovyo wakitafuta namna yakujiokoa.

Makundi ya uokoaji yapo katika eneo la tukio kutoa msaada,na watu wametahadhalishwa kutosogea katika eneo hilo na barabara kuachwa wazi.

Kwa mujibu wa Gavana wa eneo hilo Eruviel Avila, amesema kuwa kwa sasa nguvu kubwa imeelekezwa kuwasaidia majeruhi na kuwapatia huduma.

Naye Rais wa Mexico, Enrique Pena Nieto,kupitia ukurasa wake wa tweeter ametoa pole kwa familia zilizopoteza wapendwa wao kutokana na mlipuko huo na majeruhi.

Soko hilo la San Pablito mwaka 2005 lilikumbwa kasa kama huo,pale mfulilizo wa milipuko na moto mkubwa ulipozuka wakati taifa ilo liijiandaa kwa sherehe za uhuru.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles