27.1 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Mlipuko waua polisi 11 Uturuki

turkeyANKARA, Uturuki

ASKARI wa Jeshi la Polisi 11 wameuawa kwa mlipuko wa bomu uliotokea jana kwenye kituo cha polisi kilichopo katika mji mdogo wa Cizre nchini Uturuki.

Kwa mujibu wa DW, mlipuko huo umesababisha uharibifu mkubwa katika eneo hilo huku watu zaidi ya 78 wakiripotiwa kujeruhiwa vibaya.

Taarifa hiyo ambayo pia ilirushwa na kituo cha televisheni cha NTV cha  nchini humo, kulionekana moshi mzito ukifuka baada ya mlipuko huo hivyo kusababisha changamoto kwa askari wa kikosi cha zima moto kutuliza moto uliokuwa unateketeza baadhi ya majengo yaliyopo karibu na eneo ambalo  kituo hicho.

Baada ya kufanikiwa kuzimwa kwa moto, baadhi ya picha zilizokuwa zinarushwa kwenye vyombo vya habari zilionyesha uharibifu mkubwa wa ofisi ya jengo hilo.

Taarifa zaidi kutoka nchini humo zinatanabaisha kuwa takribani  majeruhi tisa wamepoteza maisha baada ya kufikishwa hospitali.

Shirika la habari la taifa, Anadolu limetupa lawama ya shambulizi hilo kwa wapiganaji wa chama cha wafanyakazi wa Kikurdi cha PKK ambao wamekuwa wakifanya mashambulizi ya mara kwa mara tangu makubaliano ya kuweka chini silaha baina yake na Serikali kuvunjika Julai mwaka huu.

Katika tukio lingine lililotokea Alhamisi jioni, jeshi la Uturuki lilishambulia eneo la ngome ya waasi la Kaskazini mwa Syria.

Mapema jana shirika la habari la Anadolu, limesema hatua hiyo ilitekelezwa baada ya waasi kukaidi matakwa ya kuwataka waondoke eneo la Mashariki.

Jeshi la Uturuki lilivurumisha makombora yake katika kikosi kiitwacho ‘People’s Protection Units (YPG)’ tawi la kijeshi la muungano wa chama cha Kikurdi wa Syria (PYD).

Hata hivyo, vyanzo vya kiintelijensia vinasema kuwa wapiganaji hao hawajarejea nyuma na kuvuka Mto Euphrates kama ilivyotarajiwa na Serikali ya Uturuki na Marekani.

Kundi hilo PKK limeorodheshwa kama kundi la kigaidi na Uturuki, Marekani na Umoja wa Ulaya.

Zaidi ya watu 40,000 wameuawa tangu waasi wachukue silaha 1984. Alhamisi Waziri wa Mambo ya Ndani, Efkan alilituhumu kundi hilo kwa kuushambulia msafara wa kiongozi mkuu wa upinzani, Kemal Kilicdaroglu.

Serikali imekuwa ikililaumu kundi hilo kwa mfululizo wa mashambulizi kwa mwezi huu katika maeneo ya Kusini Mashariki. Na kundi lenyewe limekiri kuhusika na mkasa mmoja katika kituo cha polisi.

Jumatano Uturuki ilianzisha mashambulizi makubwa ya ardhini nchini Syria yakiambatana na zana kama vifaru vyenye kusaidiwa na mashambulizi ya angani kwa lengo la kuukomboa mji wa Jarablus, operesheni ambayo inahusisha vile vile wapiganaji 1,000 kwa upande wa upinzani.

Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, ameshasema kuwa operesheni hiyo inawalenga kwa pamoja kundi la Dola la Kiislamu na wapiganaji wa Kikurdi wa Kikosi cha YPG.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles