25.8 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 27, 2024

Contact us: [email protected]

MLINZI WA MUSEVENI ATOROKA NA BUNDUKI, RISASI 120

KAMPALA, UGANDA


ASKARI wa Kikosi Maalumu cha Kumlinda Rais (SFC) aliyetoroka kutoka kambi ya Kasenyi mjini Entebbe akiwa na bunduki mbili zililizojaa risasi 120 amekamatwa, vyanzo vya habari vya usalama vimesema.

Askari huyo. Denis Ogwang Ayo alitokomea kutoka kambi hiyo yenye ulinzi mkali mwanzoni mwa mwezi uliopita katika kile SFC ilichokiita utoro wa kwanza kikosini humo mwaka huu.

Chanzo cha habari, kilichoombwa kutotajwa kutokana na unyeti wa suala hilo kilisema askari huyo alitoroka na bunduki mbili aina ya SMG zilizojaa risasi 120.

Haikuweza kujulikana sababu na namna askari huyo alivyotoroka kambi wakati akiwa na silaha na sare.

Baada ya mtoweko wake, SGC ilitoa taarifa maalumu ikitaka mtu yeyote atakayemuona kuzifahamisha mamlaka husika.

Kamanda wa SFC, Brigedia Don Nabasa alisema waliweza kunasa nyayo zake mashariki wa wilaya ya Jinja ambako alikamatwa.

“Kwetu wakati unapotoroka, tunakukamata; hatusaubiri,” alisema.

Utoro mkubwa katika historia ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Uganda (UPDF, ambalo awali lilifahamika kama National Resistance Army (NRA) ulikuwa mwaka 2013 wakati askari 400 wakiwamo walinzi wa rais 37 walipotoroka.

Wimbi la kuikimbia SFC, kikosi ambacho askari wake hujivunia kuwamo ilihusishwa na kitendo cha Agosti 2012 walipopelekwa kama vibarua katika Ranchi ya Kisozi ya Rais Museveni kwa mujibu wa chunguzi zilizofanywa na vyombo vya habari.

Alipoulizwa iwapo askari hao walifanyishwa kazi ya kuwadhalilisha, Brigedia Nabasa alijibu“hapana”.

“Katika utumishi wa umma watu hutoroka kwa sababu tofauti tofauti. Yeye Ayo alitoroka kama watumishi wengine wa umma na ni utoro wa kwanza SFC mwaka huu,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles