27.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 1, 2021

Mlemavu anaswa akitorosha madini ya Tanzanite

Na Mohamed Hamad, Simanjiro


GERALD Ochuodho (47) ambaye ni mlemavu wa mguu, amekamatwa akijaribu kutorosha madini ya Tanzanite kutoka Mirerani kupeleka Arusha.

Madini hayo ambayo thamani yake bado haijajulikana, aliyaficha katika shimo la mguu wake kwa kugandisha kwa gundi na kiatu.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro, Zephania Chaula, ambaye wakati tukio hilo limetokea alikuwa akiendelea na kikao katika moja ya ukumbi uliopo Mirerani karibu na ukuta uliojengwa kuzunguka migodi hiyo alisema tukio hilo lilitokea juzi katika machimbo ya madini ya Tanzanite na taratibu za kisheria kuhusu mtuhumiwa huyo zinaendelea.

“Walemavu hao kwa kutumia hali ya maumbile yao ya ulemavu, wamekuwa wakitumika kutorosha madini hayo, nawataka wakome mara moja,” alisema.

Alisema mtuhumiwa anaishi eneo la Songambele ambaye ni mchekechaji mlemavu na siku hiyo alinaswa akiwa ameficha madini hayo miguuni maeneo ya ulemavu wake.

“Vifurushi hivyo viliwekwa katika shimo (miguuni) na kupigwa gundi ya super glue, kwa kuwa nyayo ni fupi, aliweka vifurushi vingine mbele ya miguu,” alisema.

Pia alisema thamani ya madini hayo bado haijajulikana na taratibu za kutathimini zinaendelea.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,530FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles