24.4 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Mkwasa kuteta na uongozi Yanga

THERESIA GASPER-DAR ES SALAAM

KAIMU Kocha Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa, amesema atashiriki katika kuushauri uongozi wa klabu hiyo nini ufanye wakati wa usajili wa dirisha dogo ili kukiimarisha kikosi hicho.

Usajili wa dirisha dogo kwa klabu za Ligi Kuu unatarajiwa kufunguliwa Disemba 16 na kufikia tamati Januari 16,  mwakani.

Mkwasa alikabidhiwa mikoba ya kukipika kikosi hicho cha Jangwani, baada ya  uongozi wa Yanga kumfungashia virago aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyi Mkongomani,  Mwinyi Zahera kutokana na kutoridhishwa na mwenendo katika Ligi Kuu msimu huu.

Tangu akabidhiwe timu hiyo,  Mkwasa ameiongoza Yanga kushuka dimbani mara moja ilipoikabili Ndanda na kuibuka na ushindi wa bao 1-0, mchezo uliochezwa Uwanja wa Nangwanda Sijaona,  Mtwara.

Akizungumza jijini Dar es Salaam baada ya kumalizika kwa mazoezi ya kikosi chake yaliyofanyika Uwanja wa Uhuru, alisema  timu hiyo inahitaji maboresho katika baadhi ya maeneo ili kuifanya iwe na makali zaidi.

“Sikuanza na timu tangu mwanzoni kwani alikuwepo kocha mwingine, hata hivyo nitashiriki kuushauri uongozi wapi nguvu iongezwe ila kwa sasa siwezi kuweka wazi hadi wakati sahihi utakapofika,” alisema.

Akizungumzia maandalizi ya kikosi chake kwa ujumla alisema kinaendelea kuimarika, ambapo aliwasifu wachezaji wake kwa kujituma mazoezi.

“Kikosi kipo vizuri isipokuwa Lamine Moro yeye  bado anasumbuliwa na majeraha, lakini wengine wanaendelea na programu ya mazoezi kama kawaida,”alisema.

Alisema ataendelea kuwapa nafasi wachezaji wanaofanya vizuri mazoezini na si kufanya mabadiliko kwa lengo la kujitofautisha na mtangulizi wake.

Yanga inashika nafasi ya 15 katika msimamo wa Ligi Kuu, baada ya kushuka dimbani mara tano, ikishinda michezo mitatu, sare moja na kupoteza mchezo mmoja hivyo kujikusanyia pointi 10.

Katika hatua nyingine, Yanga itashuka dimbani leo
kuumana na Coastal Union katika mchezo wa kirafiki wa kujipima ubavu utakaochezwa dimba  la Uhuru, Dar es Salaam.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles