29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Mkwasa aita 25, awatema Cannavaro, Msuva

CHARLES BONIFACE MKWASANA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM

KOCHA mkuu wa timu ya soka ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Charles Mkwasa, amewatema katika kikosi hicho nahodha wa zamani wa timu hiyo, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na kiungo Simon Msuva wa Yanga huku akiwaita Mwinyi Kazimoto wa Simba na kipa Shaban Cado wa Mwadui FC.

Jana kocha huyo alitangaza kikosi cha wachezaji 25 watakaoivaa Chad Machi 13, mwaka huu mjini Djamena katika mchezo wa kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa Afrika (Afcon) mwakani.

Mkwasa pia amemtema winga, Mrisho Ngassa, anayecheza soka la kulipwa katika klabu ya Free State Stars ya Afrika Kusini na kuwarejesha Jonas Mkude wa Simba na beki Erasto Nyoni wa Azam FC.

Wachezaji wengine walioitwa Stars ni makipa Aishi Manula (Azam ), Ally Mustapha (Yanga) na mabeki, Juma Abdul, Haji Mwinyi, Kelvin Yondani kutoka Yanga, Shomari Kapombe, David Mwantika (Azam) na Mohamed Hussein (Simba).

Viungo ni Himid Mao, Farid Mussa (Azam), Ismail Juma (JKU), Said Ndemla (Simba), Mohamed Ibrahim, Shiza Kichuya (Mtibwa Sugar) na Deus Kaseke (Yanga).

Washambuliaji walioitwa ni nahodha, Mbwana Samatta kutoka KRC Genk ya Ubelgiji, Thomas Ulimwengu (TP Mazembe), John Bocco (Azam), Elias Maguli (Stand United), Jeremia Mgunda (Tanzania Prisons) na Ibrahim Ajib (Simba).

 Akizungumza Dar es Salaam jana wakati wa kutangaza kikosi hicho, Mkwasa amewaomba wachezaji walioitwa kujiweka fiti kwenye mazoezi wanayofanya ndani ya klabu zao kwani hakutakuwa na muda wa kufanya mazoezi kujiandaa na mchezo wa ugenini.

“Michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara na mechi za kimataifa za Klabu Bingwa Afrika na Kombe la Shirikisho barani Afrika zitachezwa kati ya Machi 18 na 20, hivyo wachezaji wote watakuwa na majukumu katika timu zao na muda wa kufanya mazoezi ya pamoja hautakuwepo.

“Ndio maana nasisitiza kwa wachezaji niliowachagua wahakikishe wanajilinda wenyewe na kujiweka fiti wanapokuja kwenye safari ya kwenda Chad,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles