28.6 C
Dar es Salaam
Saturday, January 28, 2023

Contact us: [email protected]

MKUU WA MAJESHI AAPISHWA LEO

Asha Bani

-DAR ES SALAAM

RAIS Dk. John Magufuli, leo amemwapisha Mkuu mpya wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Venance Mabeyo.

Mebeyo aliteuliwa Februari 2, mwaka huu na Amiri Jeshi Mkuu Rais Dk. John Magufuli kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Jenerali Davis Mwamunyange, ambaye amestaafu kazi Januari 31, mwaka huu.

Mbali na hilo, Rais Magufuli alimteua Meja Jenerali James Mwakibolwa kuwa Mnadhimu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania.

Pamoja na kuteuliwa kuwa Mnadhimu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Meja Jenerali James Mwakibolwa amepandishwa cheo na kuwa Luteni Jenerali.

Luteni Jenerali James Mwakibolwa amechukua nafasi iliyoachwa wazi na Jenerali Venance  Mabeyo, ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania.

Januari 30, mwaka jana Rais Dk. John Magufuli , alimuongezea muda wa mwaka mmoja Mkuu wa  Majeshi ya Ulinzi nchini,Jenerali David Mwamunyange, ambaye amekamilisha muda wake Januari 31, mwaka huu kwa mujibu wa katiba na sheria.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles