25 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 6, 2022

Contact us: [email protected]

Mkuu wa Magereza Dodoma amtibua Majaliwa

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa

Na MWANDIHI WETU, DODOMA

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana kuchunguza ni kwa nini Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dodoma, Antonino Kilumbi amekwenda kutengeneza madawati kwa watu binafsi  badala ya karakana ya Magereza kama  ilivyoagizwa na Serikali.

Magereza Mkoa wa Dodoma ilipewa Sh milioni 24 na Serikali  kutengeneza madawati 480 na kila moja lilitakiwa kugharimu Sh 50,000.

Uongozi wa gereza hilo ulitengeneza madawati hayo kwa watu binafsi ambako dawati moja limegharimu Sh 70,000.

Majaliwa alitoa kauli hiyo jana  alipotembelea Gereza la Isanga mjini Dodoma akiwa kwenye ziara ya kukagua maeneo yanayotoa huduma za jamii mjini hapa.

Alisema kama gereza hilo halikuwa na uwezo wa kutengeneza madawati hayo kwa nini kazi hiyo isingepelekwa  kwenye taasisi nyingine ya umma.

Kwa sababu hiyo alimtaka Rugimbana kufuatilia ziada ya Sh 20,000 kwenye utengenezaji wa kila dawati ilitoka wapi na ilikwenda kwa nani.

“Nimesikia kwamba mnawachangisha askari kiasi kilichoongezeka kwenye utengenezaji wa madawati hayo. Ni marufuku askari kutoa fedha mifukoni mwao kulipia shughuli za Serikali.

“Serikali imeandaa utaratibu wa kuwezesha taasisi zake zikiwamo za jeshi kwa kuzipa kazi ya kutengeneza bidhaa na miundombinu mbalimbali ikiwamo madawati ili kuziongezea tija,” alisisitiza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,606FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles