25.2 C
Dar es Salaam
Monday, August 15, 2022

Mkutano wa taasisi za fedha kufanyika Arusha

Mwandishi wetu

Mkutano wa taasisi za fedha nchini ulioandaliwa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwa kushirikiana na Umoja wa Mabenki Tanzania (TBA) unatarajiwa kufanyika jijini Arusha Novemba 21 na 22 mwaka huu kujadili namna ya kuchochea maendeleo ya sekta ya fedha nchini.

Taarifa iliyotolewa na Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki imesema mkutano huo wa 19 wa taasisi za fedha utahudhuriwa na washiriki wapatao 300 wakiwemo Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango, mawaziri, wakuu wa taasisi za fedha, wachumi waliobobea, wanataaluma na washirika mbalimbali wa maendeleo.

Katika mkutano huo zitajadiliwa mada mbalimbali zikiwemo Matumizi ya teknolojia katika kukuza sekta ya fedha ili kuleta mapinduzi ya viwanda, maeneo yenye fursa za uwekezaji katika sekta ya fedha na vigezo vinavyochangia kujenga tabia za ukopaji.

Aidha washiriki wa mkutano huo watajadili jinsi ya kukinga vihatarishi katika sekta ya fedha, namna ya kuoanisha sekta ya fedha na maendeleo ya viwanda na thmini ya mchango wa sekta ya benki katika huduma jumuishi za kifedha nchini.

Mkutano wa 18 wa taasisi za fedha ulifanyika mwaka 2016 jijini Arusha na mada kuu katika mkutano huo ilikuwa ni Jinsi sekta ya fedha inavyoweza kuifanya Tanzania inufaike kiuchumi kutokana na uwepo wake kijiografia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,784FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles