30.6 C
Dar es Salaam
Saturday, November 23, 2024

Contact us: [email protected]

Mkutano wa ‘Siku ya Afrika’ wafanyika

PRETORIA, AFRIKA KUSINI

BARAZA la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika (AU) limefanya mkutano wa kuadhimisha Siku ya Afrika kwa njia ya video na kutoa wito kwa Waafrika kuimarisha uhusiano wao ili kufikia maendeleo na amani.

Mkutano huo ulifanyika Jumatatu chini ya kauli mbiu ya ‘Kuzima Sauti ya Silaha- Kuandaa Mzingira Mema ya Ustawi wa Afrika na Kuimarisha Vita Dhidi ya CovidD-19.’

Akihutubu katika kikao hicho, mwenyekiti wa zamu wa AU ambaye pia ni Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, alitoa wito kwa nchi zilizoendelea, mashirika ya kimataifa na kikanda pamoja na wadau wa hisani kutoa msaada kwa nchi zenye uwezo mdogo katika kukabiliana na janga la maambukizi ya Covid-19, hasa nchi za Afrika. 

Pia alipendekeza kutungwa sera zenye nguvu za kuchochea uchumi, ikiwa ni pamoja na kupunguza au kusamehe madeni, na kusisitiza tena kuondolewa vikwazo dhidi ya Zimbabwe na Sudan bila masharti yoyote.

Wakati huo huo, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) Antonio Guterres amesema Afrika imeonyesha uwezo wake mzuri wa uongozi kwenye mapambano dhidi ya janga la Covid-19.

Hata hivyo, alisema vita bado vinaendelea kwenye nchi nyingi barani humo, na kutoa wito kwa nchi mbalimbali zisimamishe vita ili kushinda virusi vya corona kwa pamoja.

AP

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles