24.4 C
Dar es Salaam
Thursday, September 19, 2024

Contact us: [email protected]

Mkutano Mkuu Faida Fund kufanyika Jumamosi

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

Mkutano mkuu wa kwanza wa mwaka wa Mfuko wa Uwekezaji wa Faida (Faida Fund) utafanyika Agosti 10, 2024 mkoani Dar es Salaam.

Mkutano huo ni wa kwanza tangu kuanzishwa kwa Mfuko wa Faida unaolenga kutoa fursa kwa wawekezaji wote wa mfuko kupokea na kujadili taarifa ya fedha kwa kipindi cha mwaka unaoishia Juni 30, 2023.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Agosti 6,2024, Afisa Mtendaji Mkuu wa Watumishi Housing Investment (WHI), Dk. Fred Msemwa amesema katika kipindi cha muda mfupi WHI kupitia Mfuko wa Faida imeweza kuweka msingi imara utakaowezesha kuziba ombwe la wawekezaji wadogo kushindwa kushiriki kwenye uwekezaji katika masoko ya fedha na kupata faida.

Amesema Mfuko wa Faida umeweza kufanya mambo makubwa ikiwemo kuwa mfuko wa kwanza Tanzania, kushusha kianzio cha kuwekeza kuwa angalau Sh 10,000 na kuwawezesha wawekezaji wote hata wale wadogo kupata faida shindani na sawia katika soko.

“Tangu kuanzishwa kwa mfuko wa Faida Fund  mtaji wake umekuwa  tofauti na tulipoanza kipande kilikuwa kina thamani ya Sh 100 lakini sasa ni Sh 117. Kiwango chetu kuanzia  kuwekeza kimechochea uwekezaji katika soko la fedha, tuna wawekezajj wadogo ambao wanaweza kuwekeza kuanzia Sh 10,000 na wakaendelea kuwekeza wakiwa na 5,000.

“Pia tumebuni mfumo ambao unawezesha wawekezaji  kuwekeza na kupata faida na kuuza vipande vyake bila kufika ofisini kujaza fomu,” amesema Dk. Msemwa.

Ameeleza kuwa wakati wakitimiza mwaka mmoja mfumo huo umeweza kufikia hata watu waliopo kijijini, wanaonufaika na huduma hiyo.

Kwa upande wake Mwangalizi wa mfuko huo kutoka CRDB, Marry Mponda amewatoa hofu wawekezaji na kusema fedha zao ziko sehemu salama.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles