22 C
Dar es Salaam
Friday, August 12, 2022

Mkutano CUF waingia shubiri baada ya kukaidi amri ya polisi

Nora Damian, Dar es Salaam

Mkutano Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), upande wa Profesa Ibrahim Lipumba, umesimama baada ya kutokea kutoelewana baina ya viongozi wa chama hicho na Jeshi la Polisi.

Kwa mara ya pili jeshi la polisi limefika katika ukumbi wa Lekam unakofanyika mkutano huo na kuwazuia kuendelea likisisitiza kuna zuio la mahakama.

Difenda mbili zikiwa na askari polisi na gari moja ya maji ya kuwasha zilifika kisha Mkuu wa Polisi Wilaya ya Buguruni (OCD), Adam Maro, alionekana akizungumza na viongozi wa chama hicho.

“Hata kama umekuja na zuio la mahakama sisi hatulipokei kwa sababu wewe huna mamlaka ya kulileta na hapa hatuondoki mkitaka mtuue wote,” alisikika mmoja wa viongozi wa Cuf akimweleza OCD huyo.

Baada ya muda OCD huyo alitoka nje ya geti kisha alirudi tena akiwa ameongozana na askari wengine na kuingia ndani ukumbini.

Hata hivyo baada ya kuingia tu wafuasi wa Cuf walimtoa nje na kusababisha wajumbe wengine waliokuwa ndani kutoka.

Muda mfupi baadaye Profesa Lipumba alitoka ukumbini na kwenda kuzungumza na polisi hao kisha alionekana akiongea na simu huku akirudi ndani.

Hadi sasa polisi bado wapo katika viwanja hivi na wajumbe wa mkutano wako nje.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,504FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles