28.7 C
Dar es Salaam
Wednesday, January 19, 2022

Mkurugenzi Jamii Forums ana kesi ya kujibu

Patricia Kimelemeta, Dar es Salaam

Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jamii Forums, Maxence Melo na mwenzake Mike Mushi, wamekutwa na kesi ya kujibu katika kesi ya kuzuia jeshi la polisi kufanya uchunguzi, inayowakabili viongozi wa mtandao huo.

Washitakiwa hao wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu  leo Ijumaa Februari 22, wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutolewa uamuzi kama  wana kesi ya kujibu au la, baada ya upande wa jamhuri kufunga ushahidi wa mashahidi watatu.

Akisoma uamuzi huo, Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba amesema baada ya kupitia ushahidi na kielelezo ambacho kilitolewa mahakamani hapo amejiridhisha pasi na shaka kuwa washtakiwa hao wana kesi ya kujibu.

Amesema washtakiwa hao wanaweza kujitetea kwa kula kiapo, bila kiapo au kukaa kimya na kusubiri uamuzi wa mahakama.

Hata hivyo, washtakiwa hao wamedai kuwasilisha mashahidi watano katika kesi hiyo ili waweze kutoa ushahidi wao.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
175,312FollowersFollow
531,000SubscribersSubscribe

Latest Articles