28.1 C
Dar es Salaam
Friday, October 11, 2024

Contact us: [email protected]

Mkurugenzi Itigi, wengine sita washikiliwa kwa tuhuma za mauaji

Na SEIF TAKAZA

– SINGIDA

MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya Itigi, Pius Luhende na watu wengine sita, wanashikiliwa na   polisi mkoani Singida kwa mahojiano kuhusu kuuawa kwa Isaka Petro (28), aliyefyatuliwa risasi akiwa kanisani Februari 2.

Akizungumza na waandishi wa habari   jana, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Singida, Sweetbert  Njewike, alisema Petro aliuawa wakati maofisa saba wa Halmashauri ya Itigi wakiongozwa na Luhende, walipokuwa wakiwatafuta watuhumiwa walioharibu mali Februari mosi.

Alisema katika uharibifu wa mali, Rose Andrew alidai aliharibiwa mali yake iliyopo kwenye shamba la Tanganyika Packers ambalo linamilikiwa ha halmashauri hiyo.

“Februari 2, saa 8.30 mchana huko katika Kijiji cha Kaskazi Kata ya Kaskazi Tarafa ya Itigi Wilaya ya Manyoni, , Isaka Petro ambaye ni Msukuma na mkulima mkazi wa kijiji hicho, alifariki dunia papo hapo baada ya kupigwa na kitu chenye ncha kali kinachodhaniwa ni risasi upande wa kisogoni, wakati akiwa kwenye ibada na waumini wenzake wa Kanisa la Sabato  kijijini hapo,’’ alisema Kamanda Njewike.

Aliwataja wanaoshikiliwa na polisi kuwa ni Silvanus Lungisha (50), ofisa kilimo wa halmashauri hiyo mkazi wa Majengo Itigi na Elik Poul, ofisa sheria mkazi wa Itigi mjini.

Wengine ni Eliutha Augustino, ofisa tarafa wa Itigi mkazi wa Itigi, Yusuph John, ofisa mtendaji kijiji cha Kaskazi, Rodney  Elias, askari wanyama pori na Mkoye Steven. askari wanyama pori, walioajiriwa na Halmashauri ya  Itigi.

  Kamanda Njewike alieleza kwamba maofisa hao wa halmashauri ya Itigi, walipopata taarifa ya kuwa baadhi ya watuhumiwa wa   kuharibu mali walikuwa katika Kanisa la Wasabato  kijijini hapo,   walikwenda kwa lengo la kuwakamata.

Wakiwa katika eneo hilo, Mkurugenzi Luhende alipoingia ndani ya kanisa hilo kulitokea vurugu ndipo akatoka nje akawafungia waumini waliokuwa kwenye kanisa hilo wakifanya ibada.

Baada ya tukio hilo askari wa wanyama pori alipitia dirishani akafyatua risasi na kumpiga kisogoni Isaka na kufariki dunia papo hapo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles