23.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Mkurugenzi Hanang akemea vitendo vya kikatili

Mohamed Hamad, Hanang

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang, Bryceson Kibasa amekemea vitendo vya kikatili vinavyoendelea wilayani Hanang mkoani Manyara na kutaka vitafutiwe ufumbuzi ili wananchi waondokane na madhara yanayoendelea kujitokeza kila siku.

Kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2015/16, ukeketaji unaongoza kwa asilimia 58, ukiambatana na mimba za utotoni, vipigo, ubakaji, utakaso wa wajane na ndoa za utotoni.

Akizungumza na wasaidizi wa Kisheria katika mafunzo yaliyoandaliwa na Asasi ya HALISO kwa kushirikiana na Chama cha Wanasheria Wanawake (WLAC) amesema anaamini mabadiliko hayo yatatokana na kupatikana elimu kwa jamii.

“Nilipofika hapa miaka mitatu iliyopita niliambiwa huko ni eneo la wafugaji hawapendi elimu, nataka kuwahakikishia kuwa si kweli.

“Mwamko wa wazazi kwa sasa ni mkubwa sana, tumejipanga kuwa hata wanaokuja na taarifa za matokeo mabovu shuleni na kueleza sababu kuwa ni mwamko mdogo tunakataa na kushauri zifutwe,” amesema Kibasa.

Pamoja na mambo mengine, amesema kuna vitendo vinavyojitokeza kwa baadhi ya wazazi kufanya makubaliano watoto wao kwenda kufanya kazi za ndani mijini na kuacha haki zao za kupata elimu na ukeketaji kwa wanawake na watoto wa kike tena wakiwa wadogo vikome.

Kwa upande wake Mratibu wa Uwezeshaji Jamii Kisheria, Kituo cha Msaada wa Sheria wa Wanawake na Watoto, Consolata Chikoti amesema ili kamati hiyo iwe na mafanikio jamii inatakiwa kutoa ushirikiano, wasiwaone maadui, wajue kuwa wana nia njema ya kusaidia jamii na pia mpango kazi wa taifa ujulikane kwa wadau wote.

“Tumeamua kuja Hanang na kutoa mafunzo hayo kwa sasabu tumeona hii jamii ina uhitaji wa aina yake, ina watoto wenye vipaji, lakini kuna vikwazo vikiwemo mila na desturi kandamizi kwa watoto wa kike na wanawake,” amesema.

Amesema katika kukabiliana na vitendo hivi vya kikatili suala la ushahidi nalo limekuwa kikwazo, kwani sheria ina mapungufu makubwa, kuna matatizo mengine yanahitaji mbinu mbadala ikiwemo sheria yenyewe, na kudai pamoja na Serikali kupanga bajeti kutekeleza mpango huu, bado ina mambo mengi, hivyo wadau tajwa waone haja ya kuchangia kufanikisha zoezi hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles