Mkufunzi Chuo cha Ardhi kusaidia ujenzi shule ya msingi

0
1133

ERICK MUGISHA, DAR ES SALAAM

Mkufunzi wa Chuo kikuu cha Ardhi, Prof. Nancy Maroble ameahidi kushirikiana na shule ya Msingi ya Mtakatifu James katika ujenzi wa karo la kufanyia mitihani ya taifa ili waweze kuepukana na kero hiyo ambayo imekuwa ikiwasumbua kwa muda mrefu.

Akizunguza katika mahafali ya darasa la saba yaliyofanyika shuleni hapo, prof. Maroble alisema uongozi wa shule ukianzaa ujenzi wa karo la wanafunzi anaomba aweze kushirikiana nao kutokana na kutaka wanafunzi kusoma kwenye mazingira mazuri.

Alisema wanafunzi wanakosa karo la kufanyia mitihani ya taifa ya darasa la saba na darasa la nne hivyo hana budi kushirikiana na uongozi wa shule hiyo kwakuwa wanafunzi huonesha juhudi katika ufaulu kwenye mitihani yao kwa wilaya, kimkoa na hata kitaifa kila mwaka.

“Tunawaomba sana wazazi kuweza kukamilisha ada za karo ya shule ili kutatua matatizo kama haya  na kuweza kuona wanafunzi wanasoma kwenye mazingira mazuri,”

 “Wazazi mnatakiwa kuonesha ushirikiano baina yenu na walimu katika kujua maendeleo ya wanafunzi katika taaluma ya kielimu hata kinidhamu hapa shuleni”, alisema Prof. Maroble.

Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Peter Ngichogo alisema wapo mbioni katika kuanza ujenzi wa karo la kufanyia mitihani na mabweni ya kulala wanafunzi.

Alisema wanafunzi hawana mabweni ya kulala hivyo wanalazimika kuwa na kambi kwa muda kwaajili ya kuwandaa wanafunzi wanao tarajia kufanya mitihani ya taifa wa darasa la saba na la nne.

“Walimu wa shuleni hapa si wakuhama na wamedumu kwa muda mrefu kwajili ya mikakati ya kuweza kutoa Elimu ya hali ya juu na nidhamu kwa wanafunzi”, alisema mwalimu Ngichongo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here