Mkude kuikosa Equatorial Guinea

0
902

Mwandishi Wetu

Kocha wa Timu ya taifa ‘Taifa Stars’, Etiene Ndayiragije amemruhusu kiungo wa klabu ya simba Jonas mkude kuondoka kwenye kikosi hicho kwenda kushughulikia masuala yake ya kifamilia.

Mkude alitoa taarifa kwa kocha Ndairagije kuomba ruhusa ya kutojiunga ili kushughulikia masuala ya kifamilia, ruhusa ambayo alipewa kabla ya kuanza kwa kambi.

Kulingana na muda mfupi uliobaki kuelekea mchezo dhidi ya Equtial Guinea, ndayiragije hataweza kuongeza mchezaji mwingine.

Taifa Stars inatarajia kuumana na Equtial Guinea Ijumaa Novemba 15, Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam katika mchezo wa kwanza kufuzu hatua ya makundi Afcon 2021.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here