23.3 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

MKUDE, KOTEI MAJARIBUNI SIMBA

  • Washushiwa kiungo mzoefu, kupaa na msafara Uturuki

NA JOHN DANDE-DAR ES SALAAM


SIMBA imedhamiria kujijenga kiasi cha kutosha kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara sambamba na ushiriki wake katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika,  baada ya kumshusha nchini kimyakimya kiungo Mzambia, Clatous Chama.

Kiungo huyo msimu uliopita aliichezea Al Ittihad Alexandria ya nchini Misri.

Clatous alitarajiwa kusaini mkataba wa kuwachezea Wekundu hao baada ya kukamilisha zoezi la uchunguzi wa afya yake lililofanyika jana sambamba na  wachezaji wengi wa timu hiyo.

Ujio wa Clatous katika kikosi cha Simba  ni wazi utazidisha ushindani wa namba katika idara ya kiungo ya timu hiyo, ambayo pia ina wakali wengine wakiwamo, Jonas Mkude, Muzamir  Yassin, Said Ndemla na James Kotei.

Kotei na Mkude ndio walikuwa wakiaminiwa zaidi katika eneo la kiungo la Simba katika Ligi Kuu msimu uliopita.

MTANZANIA lilimfumania Chama akiwa miongoni mwa wachezaji wa Simba waliofika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya afya.

Zoezi hilo lilianza mapema asubuhi na kuendelea hadi jioni chini ya daktari wa timu hiyo, Edward Bavu, ambapo wachezaji wa timu hiyo walifanyiwa vipimo mbalimbali ikiwemo vile vya moyo.

Simba iko kwenye maandalizi ya mwisho kabla ya safari ya nchini Uturuki kesho ambako itapiga kambi ya kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Simba tayari imekamilisha usajili wa wachezaji Meddie Kagere kutoka Gor Mahia ya Kenya akiwa ni raia wa Rwanda, Adam Salamba kutoka Lipuli ya Iringa na Mohamed Rashid kutoka Tanzania Prisons.

Juzi uongozi wa klabu hiyo ulimtangaza raia wa Ubelgiji, Patrick Aussems, kuwa kocha mkuu mpya wa timu ambaye amechukua nafasi ya Mfaransa, Pierre Lechatre.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles