25.2 C
Dar es Salaam
Friday, August 12, 2022

Mkude, Dilunga wazidi kunoga Simba

MWANDISHI WETU-MWANZA

VIUNGO wa Simba, Jonas Mkude na Hassan Dilunga wamezidi  kutakata, baada ya  kila mmoja kupachika bao  katika ushindi wa mabao 4-1 ilioupata timu hiyo dhidi ya Alliance, katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa jana Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Ushindi huo ni uliifanya Simba kufikisha pointi 41 na kuzidi kung’ang’ana kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo, baada ya kushuka simbani mara 16, ikishinda michezo 13, sare mbili na kupoteza mmoja.

Katika mchezo huo, Alliance ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao la uongozi dakika ya 27 kupitiwa kwa mkwaju wa mpira wa adhabu uliopigwa na Israel Paul.

Simba ilisawazisha dakika ya 45 kupitia kwa Mkude, wakati mabao mengine ya Wekundu hao yalipachikwa na Meddie Kagere dakika ya 58, Clatous Chama dakika ya 63 na Dilunga dakika ya 78.

Mkude pia alifunga bao moja wakati Simba iliposhinda mabao 2-1 dhidi ya Mbao, katika mchezo wa ligi hiyo uliochezwa kwenye uwanja huo.

Mchezo ulivyokuwa.

Simba ilikuwa wa kwanza kufanya shambulizi kwenye lango la Alliance.

Dakika ya 13, mkwaju wa Dilunga ulipaa juu ya lango la Alliance.

Dakika ya 19, kiungo Sharaf Shiboub alipkea pasi ya  Francins Kahata na kufyatua mkwaju uliopaa juu la lango la Alliance..

Licha ya kuutawala mchezo, Simba ilijikuta ikifungwa bao dakika ya 27 kupitia mkwaju wa Patrick.

Bao hilo liliiongezea nguvu Alliance kwani dakika ya 40, kiki ya Michael Chinedu ilipaa juu ya lango la Simba.

Wakati wote huu Simba ilikuwa ikimiliki mpira zaidi ukilinganisha na Alliance ambayo ilikuwa ikifanya mashambulizi ya kushtukiza.

Dakika ya 44, kiki dhaifu ya Dilunga haikuwa na madhara kwa kipa wa Alliance, John Mwenda  kabla ya Mkude kuisawazishia Simba dakika ya 45, baada ya kuunganisha pasi ya Shiboub.

Kipindi cha pili, kilipoanza kila upande ulionekana kuingia uwanjani na mkakati wa kusaka mabao zaidi.

Dakika ya 58, Kagere aliifungia Simba bao la pili kwa kichwa baada ya kuunganisha krosi ya beki Pascal Wawa.

Bao hilo liliwaongezea mzuka wachezaji wa Simba na kufanya mashambulizi zaidi langoni mwa Alliance.

Dakika ya 63, Chama aliiandika Simba bao la tatu kwa mkwaju wa mpira wa adhabu.

Dakika ya 78, Kagere akiwa anaangaliana na Mwenda alishindwa kutumbukiza mpira wavuni baada ya mkwaju wake kutoka nje.

Dilunga alisawazisha makosa ya Kagere kwa kufunga bao la nne baada ya kupokea pasi ya Shiboub.

Licha ya Alliance kupambana ili kurudisha mabao walinzi wa Simba walionekana kuwa makini na kuzuia mashambulizi langoni mwao.

Dakika 90 za pambano hilo zilikamilika kwa Simba kutoka uwanjani kifua mbele kwa ushindi wa mabao 4-1.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,536FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles