26.2 C
Dar es Salaam
Monday, March 27, 2023

Contact us: [email protected]

Mkude, Ajibu kujiunga Stars Jumatano

THERESIA GASPER-DAR ES SALAAM

WACHEZAJI wa Simba waliojumuishwa katika kikosi cha timu ya Taifa, ‘Taifa Stars’, wanatarajia kurejea nchini kesho kutwa na kuungana na wenzao, kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa kuwania tiketi ya kushiriki fainali za mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani(Chan) dhidi ya Kenya.

Taifa Stars ilianza kambi ya maandalizi ya mchezo huo jana jioni, kwa wachezaji kuingia kambini katika hoteli ya White Sands,  jijini Dar es Salaam.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Julai 28 mwaka huu,  Uwanja wa Taifa,  jijini Dar es Salaam kabla ya ule wa marudio kupigwa Agosti 4 mwaka huu nchini Kenya.

Simba imechangiwa wachezaji saba katika kikosi hicho cha Taifa Stars, wakiwemo kipa Aishi Manula, mabeki Erasto Nyoni na Gadiel Michael, viungo Jonas Mkude, Ibrahim Ajib,Hassan Dilunga na mshambuliaji John Bocco.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Kocha Mkuu wa timu hiyo, Patrick Aussems  alisema wachezaji hao hawataathiri maandalizi yao yanayoendelea nchini Afrika Kusini.


“Tumefanya mazoezi kwa siku kadhaa wote lakini wachezaji wengine wameitwa katika timu ya Taifa na wanatarajia kuondoka Jumatano kuungana na wenzao,” alisema.

Aliwasifu wachezaji wake kwa kuwa wasikivu na kuonyesha kujituma, akisema hali hiyo itakifanya kikosi chake kuwa moto msimu ujao.

Katika hatua nyingine Kocha Msaidizi wa Taifa Stars, Seleman Matola alisema, tayari wachezaji wanaounda kikosi hicho wameanza kuingia kambini.

“Niliwasiliana na Kocha Mkuu, Ettiene Ndayiragije, aliniambia wachezaji wanatakiwa kuingia kambini leo (jana) jioni ili kuanza maandalizi,” alisema.

Wachezaji wengine waliojumuishwa katika kikosi cha Taifa Stars ni makipa Juma Kaseja (KMC) na Metacha Mnata (Yanga), mabeki ni Paul Godfrey, Kelvin Yondani (Yanga), Boniface Maganga (KMC), Idd Mobi (Polisi Tanzania), Paul Ngalema (Namungo FC)na David Mwantika (Azam FC).

Viungo ni Abdulaziz Makame, Feisal Salum ‘Fei Toto’ (Yanga), Mudathir Yahya, Abubakar Salum ‘Sur Boy’, Masoud Abdallah, Frank Domayo (Azam FC). Washambuliaji ni Salim Ayee (KMC)Iddy Seleman ‘Idd Nado’, Shaban Chilunda (Azam FC) na Kelvin John (U17

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,206FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles