22.2 C
Dar es Salaam
Thursday, September 29, 2022

MKUCHIKA: MBUNGE ASIYETAKA WAKURUGENZI KUSIMAMIA UCHAGUZI APELEKE HOJA SHERIA IBADILISHWE

Na Mwandishi wetu               |           


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora), George Mkuchika, amesema Mbunge yeyote anayeona kuwa si sahihi Wakurugenzi wa Halmashauri kutosimamia uchaguzi, apeleke hoja Bungeni ili sheria hiyo ibadilishwe.

Ametoa kauli hiyo wakati akimjibu Mbunge wa Mtambile, Masoud Abdalah Salum ambaye aliseme Wakurugenzi wa Halmashauri kishera ndiyo wasimamizi wa uchaguzi, je, serikali iko tayari kubadilisha sheria hiyo?

Akijibu hilo, Mkuchika amesema Mbunge anayeona sheria hiyo haifai apeleke hoja bungeni ili ibadilishwe.

Naye Mbunge wa Viti Maalumu, Ruth Mollel amesema Wakurugenzi hao ni wanachama wa CCM walioshindwa kwenye kura za maoni, je, serikali iko tayari kutoa kauli gani endapo wakipeleka orodha Wakurugenzi wa aina hiyo.

“Na wapo ambao wameonyesha itikadi za kisiasa je serikaki ina kauli gani,”amehoji.

Akijibu hilo, Mkuchika amesema: “Mkurugenzi yeyote unayemchagua lazima kuna chama anachokipenda, nchi zote Duniani Rais aliyepo madarakani anapanga watu wake.
“Tunayo Mahakama pale ambapo mtu anaona hakutendewa haki aende Mahakamani,”amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,204FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles