27.4 C
Dar es Salaam
Thursday, December 9, 2021

Mkubwa na Wanawe wafunika Tamasha la Sauti za Busara kwa nyimbo za Yamoto

FESTO POLEA, ZANZIBAR

Kuimba kwa umahili mkubwa idadi kubwa ya nyimbo zilizokuwa zikiimbwa na wasanii wa kundi la Yamoto, kundi la Muziki la Mkubwa na Wanawe limetoa ishara kuwa wanauwezo mkubwa wa k ukonga nyoyo za mashabiki wapenzi wa nyimbo hizo.

Kundi hilo limeonyesha uwezo mkubwa wa kuimba nyimbo hizo katika shoo yao waliyoifanya Februari 7 katika Tamasha la 16 la Kimataifa la Sauti za Busara linloendele viunga vya Ngome Kongwe, Unguja visiwani Zanzibar.

Kundi hilo limeweza kuonesha umahri wao wa kuimba na kucheza jukwaani huku wakiendana sambamba na mapigo na ala za muziki wa bendi iliyopiga live.

Vijana hao wa waliweza kuimba nyimbo zaidi ya tano (5) ikiwemo ya Stata ukiimbwa na mwanadada Catrima Wegesa huku nyimbo zingine zikiimbwa na Abdala Mustapha ‘Kisamaki’ huku kijana mdogo kabisa wa kundi hilo, Abdul Kadry ‘Dogo Kadry’ mwenye miaka 15 akiwa kidato cha kwanza alikuwa kivutio kila alipopanda jukwaani kuimba nyimbo tofauti hasa alipoimba wimbo wa Asu uliimbwa na mwanamuziki wa taarabu, Abdul Misambano.

Kundi hilo lililo chini ya Said Fella ‘Mkubwa Fella’ ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Kilungule wilayani Temek jijini Dar es Salaam hadi sasa lina vijana wanaofanya kazi za Sanaa za Muziki zaidi ya 100.

Miongoni wa wasanii waliowahi kuwa kwenye kundi la Mkubwa na wanawe ni pamoja na Dogo Aslay, Mboso, Beka Fleva, Enock Bella, Getu, Madada Sita na wengine wengi.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
168,672FollowersFollow
527,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles