MKOSOAJI WA MUSEVENI KUCHUNGUZWA AKILI

0
492

KAMPALA, UGANDA


MAHAKAMA Kuu nchini Uganda imeamuru kurudishwa gerezani na kuchunguzwa akili kwa msomi na mkosoaji mkubwa wa Rais Yoweri Museveni, Stella Nyanzi.

Mhadhiri na mtafiti huyo wa chuo kikuu alikamatwa na kuwekwa gerezani zaidi ya wiki mbili zilizopita baada ya kufunguliwa mashtaka kuhusu makosa ya mtandaoni.

Makosa hayo yanatokana taarifa alizoweka kwenye ukurasa wake wa facebook, ambako amewashambulia Museveni na mke wake Janet, ambaye ni waziri wa elimu.

Amewashutumu kwa kuvunja ahadi ya uchaguzi ya kutoa vitaulo vya wanawake kwa ajili ya kujisitiri wakati wa siku zao.

Miongoni mwa matusi anayodaiwa kuyaandika ni pamoja na kumuita Museveni ‘jozi ya makalio’ na mkewe, ‘bongo tupu.’

Msomi  huyo alikuwa amefikishwa Mahakama Kuu na kuomba dhamana baada mahakama moja ya chini kukataa kusikiliza kesi hiyo.

Pia alikuwa akiitaka Mahakama Kuu kutozingatia ombi la serikali la kutaka afanyiwe uchunguzi wa akili.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here