Mkongwe wa saxafoni Cameroon afariki kwa corona

0
1471

Mwanamuziki nguli aliyetamba kwa Muziki wa Afro Jazz na uchezaji ala ya muziki wa Saxafoni nchini Cameroon, Manu Dibango amefariki dunia leo Jumanne Machi 24, baada ya kuugua ugonjwa wa homa ya mapafu unaosababishwa na virusi vya corona.

Dibango alitambulika vyema kupitia kibao chake cha Soul Makossa alichokiimba mwaka 1972. Mwanamuziki huyo anakuwa msanii wa pili Afrika kufariki kwa ugonjwa wa corona, mwingine ni Aurlus Mabele kutoka nchini Congo aliyefariki wiki iliyopita.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here