25.4 C
Dar es Salaam
Monday, November 18, 2024

Contact us: [email protected]

Mkoa wa Kagera wapitisha bajeti ya Bilioni 346

Renatha Kipaka, Bukoba

Mkoa wa Kagera umepitisha makisio ya fedha Sh Bilioni 346 katika bajeti kuu ya mwaka wa fedha 2022/2023 katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo mkoani Kagera.

Hayo yamebainishwa na mwishoni mwa wiki na Katibu Tawala, Mipango na Usaidizi wa Uratibu mkoani humo, Nestory Bwana wakati akisoma taarifa ya makisio ya bajeti hiyo kwenye kikao cha kamati ya ushauri ya Maendeleo ya Mkoa (RCC).

Fedha hiyo imeongezeka kutoka Sh bilioni 294 kwa mwaka 2021/2022 na kufikia bilioni 346 ambayo ni makusanyo ya vyanzo vya ndani na mchango wa wadau waendeleo.

“Kwa miaka mingi kidogo fedha za maendeleo ilikuwa ilitoka kwa asilimia ndogo lakini mwaka huu,tumefika nusu mwaka na tuko asilimia 50 imeongezeka kidogo,: amesema Bwana.

Aidha amesema, shughuli zinazofanyika ni kuwepo miradi mbalimbali ya kimkakati ikiwemo ujenzi wa kituo cha magari ya mizogo kinachoendelea kujengwa kata Nyakanazi wilayani Biharamulo.

“Mfano mradi wa kituo cha magari ya mizogo inayotoka nchi jirani na kuingia mikoani pia kutoka nchini kwenda nje ambacho kimefikia asilimia 95 ya ujenzi wake,” amesema Bwana.

Ameongeza kuwa kwa mwaka wa fedha 2021/2022 shughuli zilifanyika na tayari huduma zimeanza kutolewa ikiwamo vyumba vya madarasa kwa shule za sekondari.

“Tuliangalia hadi kufikia mwezi Desemba 2021 miradi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa imekamilika na wanafunzi waliofungua Januari 17, 2022 wanatumia pamoja na Hospital za wilaya kwa wilaya zetu,” amesema Bwana.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya Bukoba, Murshid Ngeze, amesema endapo fedha ya makisio itaidhinishwa na (TAMISEMI) na viongozi kusimamia vizuri itasaidia maendeleo kwa mkoa.

Ngeze amesema yapo maeneo ambayo yanahitaji miradi ya kuendelezwa na kunufaisha wananchi wa vijijini waweze kupiga hatua kwa kupata huduma zinazotoka serikalini.

Hata hivyo, amesema huduma za maji, miradi ya ujenzi wa vyanzo vya mapato ni sehemu ya kuongeza maendeleo kwa wananchi na taifa kwa ujumla.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles