27.3 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 17, 2024

Contact us: [email protected]

Mkoa wa Dar es Salaam kuanzisha mikakati ukusanyaji wa mapato

NBRIGHITER MASAKI.

Mkoa wa Dar es Salaam, umeanza mikakati ya kuendelea kujihimarisha katika ukusanyaji wa mapato Kwa kukutanisha wataalamu wa taasisi wanazuoni, makampuni na wafanyabiashara wakubwa wanaohusika na maswala ya kifedha.

Akizungumza na wandishi wa habari leo Mei 17 Jijini Dar es Salaam, katika kikao cha kutoa maoni ya mikakati hiyo Katibu Tawala mkoa wa Dar es Salaam ,Abubakari Kunenge, amesema wamejipambanua kuweza kutumia mapato ya ndani kwa kufanya miradi mikubwa na kufanya jukumu la kumsaidia Rais.

“Tumeona tunaweza kufanya vizuri hivyo tumetumia nafasi hii kuomba makampuni, watalamu, walimu ,wafanya biashara na wadau mabalimbali watakao tusaidia kutushauri katika suala zima la ukusanyaji wa mapato na kutoa maoni yao pia kutusaidia jinsi ya kuboresha kupata mapato ya mkoa huu wa Dar Es Salaam ilikumsaidia Rais Magufuli Katika kukabiliana na miradi ya maendeleo”,amesema Kunenge.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya viwanda na biashara, Joseph Simbakaria ,ametoa pongezi kwa wafanyakazi kutoka mkoa wa Dar es Salaam wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Paul Makonda,kwa kufanya kazi nzuri ya ukusanyaji wa Mapato na kuona umuhimu wa kukaa na wadau wa biashara kuangalia jinsi gani wanaweza kusaidia mapato mkoani hapo.

“Napenda kutoa pongezi kwa wafanya kazi wa mkoa Da es Salaam wakiongozwa na Mkuu wa mkoa huo, Paul Makonda, kwa kufanya kazi nzuri ya ukusanyaji wa Mapato na kuona umuhimu wa kukaa na wadau wa biashara kuangalia jinsi gani tunaweza kusaidia mapato ya mji mkuu wa biashara japo mji mkuu ni Dodoma ila kibiashara ni Dar es salaam.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles