26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

‘MKIMBIZI’ KUTOKA KOREA KASKAZINI ‘ASHINDA’ URAIS KUSINI

SEOUL, KOREA KUSINI

WAPIGA kura wa Korea Kusini wamemchagua kwa kishindo mgombea urais wa Chama cha Kiliberali Moon Jae-in, mtoto wa mkimbizi kutoka Korea Kaskazini, kwa mujibu wa utafiti uliohusisha wapiga kura waliohojiwa (exit poll).

Matokeo hayo, ambayo wapiga kura waliulizwa mgombea waliyempigia kura baada ya kuondoka katika vituo vya kupiga kura yalimpatia Moon ushindi wa asilimia 41.4 ya kura dhidi ya asilimia 23,3 wa mhafidhina Hong Joon-Pyo.

Kwa kipindi chote cha kampeni Moon ameeleza kupendelea kufanya majadiliano na Korea Kaskazini akienda kinyume na sera za sasa zilizoachwa na Rais aliyemtangulia.

Chaguzi hizo za mapema ziliitishwa baada ya kashfa za rushwa kusababisha kutimuliwa kwa aliyekuwa Rais wa kwanza mwanamke nchini hapa Park Geun-hye.

Park alifutilia mbali uhusiano wote na Korea Kaskazini, kitendo ambacho  Moon amekipinga akisema ni sababu ya taifa hilo la kikomunisti kulimbikiza silaha tishio kwa amani eneo hilo.

Mwitikio mkubwa wa wapiga kura ulitarajiwa na iwapo ushindi wa Moon utathibitishwa anatarajia kuapishwa leo.

Akiwa ni mtoto wa mkimbizi kutoka Korea Kaskazini, Moon alifungwa jela wakati akiwa mwanafunzi katika miaka ya 1970 kwa kuongeza maandamano dhidi ya mtawala wa kijeshi Park Chung-hee – ambaye ni baba wa Park.

Baadaye alivitumikia vikosi maalumu vya Korea Kusini kabla ya kuwa mwanasheria wa haki za binadamu.

Moon kupitia Chama cha Democratic Party of Korea aliwania urais na kushindwa dhidi ya Park katika chaguzi za mwaka 2012.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles