25.4 C
Dar es Salaam
Monday, January 30, 2023

Contact us: [email protected]

MKEMIA MKUU: WANAOTUMIA DAWA ZA KULEVYA WAMEONGEZEKA

 

Na ESTHER MNYIKA

-DAR ES SALAAM

MKEMIA Mkuu wa Serikali, Profesa Samuel Manyele amesema  sampuli za watu wanaotumia dawa za kulevya zimeongezeka kwa kipindi cha miezi miwili hadi kufikia 1,000 kutoka 644 ambapo pia wanatarajia kupokea kesi za aina hiyo 3,600 hadi kufikia Desemba mwaka huu.

Aidha, kutokana na wingi wa kesi hizo hivi sasa inawalazimu kwenda Kwa Mpiga Chapa wa Serikali kuchukua karatasi za siri ili kuepuka kuvuja kwa majibu hayo na wafanyakazi kulipwa malipo ya ziada kutokana na kufanya kazi kwa saa 18.

Takwimu hizo za Mkemia Mkuu zimekuja muda mfupi baada ya hivi karibuni Mkuu wa Dar es Salaam, Paul Makonda kutaja watu wanaotuhumiwa kujihusisha na uuzaji na utumiaji wa dawa za kulevya  ambapo katika orodha hiyo aliwataja baadhi ya wasanii, wanasiasa, viongozi wa dini na wafanyabiashara.

Profesa Manyele amesema hayo leo wakati akitoa taarifa ya serikali kuhusu ununuzi wa  mtambo wa kisasa wa kupima sampuli tofauti unaoitwa 'energy Dispersive X-Ray Flourescence SPectrometer' (EDXRF) ambao umegharimu Sh milioni 101.7.   

“Kutokana  ongezeko la kupima sampuli za dawa za kulevya tunalazimika kusitisha kupima sampuli nyingine kwa lengo la kuwahisha majibu ya watuhumiwa wanaoshikiliwa na vyombo  vya usalama ili hatua za kisheria  zichukuliwe, hivyo kutokana na ongezeko la kesi hizo, tumeanzisha kitengo maalumu kwa ajili ya kupokea kesi za dawa za kulevya tu ili kurahisha majibu ya kesi hizo kupatikana kwa wakati na kufanyia  matengenezo  mitambo husika,” amesema Profesa Manyele.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles