31.2 C
Dar es Salaam
Friday, October 11, 2024

Contact us: [email protected]

MKE WA RAIS WA ZAMANI MAREKANI AFARIKI DUNIA

TEXAS, MAREKANI


MKE wa aliyekuwa Rais wa Marekani, George H. W. Bush, ambaye pia ni mama wa Rais mwingine wa zamani wa nchi hii George W. Bush, Barbara, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 92.

Katika miaka ya karibuni afya yake ilikuwa ikidhoofu na kulazwa muda mrefu hospitalini kabla ya kuamua kuacha kuendelea kutumia dawa, kwa mujibu wa taarifa ya ofisi ya familia yake.

Barbara aliheshimiwa na kambi zote za kisiasa nchini Marekani, na amesifiwa na Rais Donald Trump kama mtetezi wa familia imara.

Ndoa ya Barbara na mumewe ilidumu kwa miaka 73.

Trump ameamuru bendera zote za Marekani kupepea nusu mlingoti kumuenzi marehemu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles