MKE WA MZEE MAJUTO ALIA KUFUKUZWA TANGA

0
1982


WIKI mbili baada ya kuzikwa kwa mchekeshaji mahiri Bongo Mzee Majuto, mke wake Aisha Yusuph, amesema maneno ya ndugu wa marehemu yamemfanya ahame katika nyumba ya mumewe iliyopo Donge, Tanga na kurudi kwao Vingunguti. Dar es Salaam.

Aisha ambaye alifunga ndoa mwaka 1997 na kufanikiwa kupata watoto wanne na Mzee Majuto, anasema aliambiwa na ndugu wa marehemu kuwa hatasaidiwa kwa chochote.

Baada ya madai hayo Swaggaz, lilimtafuta mjomba wa Mzee Majuto Hamza Kasongo ambaye alisema hawezi kusema chochote mpaka siku ya 40 itakapofika Septemba 14 mwaka huu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here