25.2 C
Dar es Salaam
Sunday, April 2, 2023

Contact us: [email protected]

Mke wa mchungaji ajinyonga  kanisani

Na Ibrahim Yassin-Ileje

MKE wa Mchungaji wa Kanisa la Last, Rusajo Mwambene (40), amekutwa amefariki dunia kwa kujinyonga kwa kamba ndani ya kanisa hilo, lililopo Kijiji cha Shilinga, wilayani Ileje, mkoani Songwe, kwa sababu zisizoeleweka.

Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo, Selina Kayange, alisema kuwa, mwanamke huyo anadaiwa siku za hivi karibuni alijifungua mtoto ambaye alifariki dunia.

Alisema baada ya mtoto huyo kuzikwa, bado mwanamke huyo alikuwa akienda makaburini kila siku ambako alikuwa akilia.

Hata hivyo, wiki iliyopita alitoweka nyumbani kwake na kuanza kusakwa kila mahali, ambapo jana mwili wake ulikutwa ndani ya kanisa huku akiwa ananing’inia kwa kujinyonga kwa kamba.

“Kitendo cha kuchukua uamuzi wa kujinyonga kwa kweli ni jambo gumu sana na lisilompendeza Mungu. Ni tukio ambalo limetushangaza sana, hivi kweli mke wa mchungaji unafikia hatua hii nzito, hapana hakustahili kufanya hivyo,” alisema Kayange.

Akizungumzia tukio hilo jana, Ofisa Mtendaji wa Kata ya Ngulilo, Nickodemas Yanga,  alikiri kuwepo kwa tukio hilo na kusema kuwa alipata taarifa kutoka kwa uongozi wa kijiji, naye alitoa taarifa kwa uongozi wa wilaya ambao walifika katika eneo hilo kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi na kuchukua mwili huo kwa uchunguzi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,407FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles