26.9 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Mkazi Chanika akabidhiwa pikipiki ya NMB Bonge la Mpango

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

WATEJA wa NMB walioibuka washindi wa pikipiki za mizigo aina ya Skymark katika droo za msimu wa pili wa Kampeni ya Weka Akiba na Ushinde ‘NMB Bonge la Mpango – 2merudi Tena,’ wameendelea kukabidhiwa zawadi zao, jana ikiwa ni zamu ya Bileshi Hamisi, wa Chanika, Dar es Salaam.

NMB Bonge la Mpango ni kampeni ya miezi mitatu (Oktoba hadi Desemba 2021), iliyokuwa ikihamasisha utamaduni chanya wa kuweka akiba, ambako kila wiki washindi 12 walizawadiwa, 10 kati yao wakitwaa pesa taslimu na wawili wakijinyakulia pikipiki za Skymark zenye thamani ya Sh milioni 4.5 kila moja.

Zawadi zenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 237, zikiwamo pesa taslimu na pikipiki 50, zilitolewa katika kampeni hiyo iliyofikia tamati Desemba 30, mwaka jana, ambako mfululizo wa kuwakabidhi pikipiki hizo umeendelea, hafla ya kumkabidhi Bileshi, ilifanyika tawini kwake Kisarawe mkoani Pwani.

Akizungumza kabla ya kukabidhi pikipiki hiyo kwa Bileshi, Meneja wa NMB Tawi la Kisarawe, Justina Kikuli, alisema kampeni hiyo iliyolenga kuchagiza utamaduni wa kufungua akaunti na kuweka akiba, sambamba na kurejesha kwa jamii sehemu ya faida yao kwa mwaka uliopita, ilikuwa ya mafanikio makubwa.

“Bonge la Mpango ni kampeni iliyofanyika kwa mafanikio, huku ikiwanufaisha wengi. Tunawashukuru wateja wetu wa zamani pamoja na wapya waliofungua akaunti na kuweka kianzio angalau cha Sh 100,000. Pia tunawapongeza walioshinda zawadi, akiwemo Bileshi ambaye ni mteja wa tawi letu la Kisarawe,” amesema Kikuli.

Kwa upande wake, Bileshi alikiri kuwa na furaha isiyoelezeka kwa kukabidhiwa pikipiki hiyo ya mizigo na kwamba awali alipopigiwa simu kufahamishwa juu ya ushindi wake, hakuamini kirahisi, lakini makabidhiano hayo yamempa uhakika kuwa kampeni ilikuwa ikiendeshwa kihalali na wenye bahati ndio walioshinda.

“Naishukuru NMB kwa zawadi hii, haikuwa rahisi kuamini kuwa kweli simu ya ushindi ilitoka kwao, nilihisi ni matapeli wa mitandaoni, lakini hatimaye leo hii nimekabidhiwa zawadi yangu. Wito kwa Watanzania ni kuendelea kuitumia NMB ili kukuza faida za akiba zao, lakini pia kunufaika kwa zawadi kama hizi,” amesema.

Katika makabidhiano hayo, Bileshi aliambatana na mkewe Masha Ally, ambaye alifichua kwamba alikuwa kwenye wakati mgumu kwani majirani, ndugu, jamaa na marafiki wa familia yao waliwacheka sana walipotangaza kupigiwa simu ya ushindi huo, huku wakiambiwa wajiandae kutapeliwa, kauli zilizowakatisha tamaa.

“Tulijisikia aibu kusemwa vibaya mtaani, ambako tukitazamwa kama washamba tusiojua mbinu za matapeli wa mitandaoni, lakini leo hatimaye mume wangu anakabidhiwa zawadi yake hii. Niwashukuru NMB kwa hili na niwaambie Watanzania kuwa hakuna utapeli wala upendeleo katika kampeni hizi,” amesema Masha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles