33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

MKATABA WA TICTS WAFUMULIWA BANDARI

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa

Na ASHA BANI-DAR ES SALAAM

MAMLAKA ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) na Kampuni ya kimataifa ya kupakua na kupakia makasha Tanzania (TICTS), zimesaini mkataba mpya baada ya majadiliano yaliyochukua miezi saba kufikia makubaliano.

Marekebisho hayo yamefanyika baada ya maagizo ya Rais Dk. John Magufuli kutembelea Bandari ya Dar es Salaam kukagua utendaji na kutoa maagizo kwa waziri mwenye dhamana kushughulikia upungufu wa TICTS ili waweze kuendelea na shughuli hizo.

Akizungumza jana Dar es Salaam baada ya hafla ya kusaini mkataba huo, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, alisema mkataba huo mpya umeondoa masharti hasi ambayo yalikuwa yanabana masilahi kwa Tanzania.

Alisema kwa sasa TICTS watalipa kodi ya mwaka ya Dola za Marekani milioni 14 kutoka milioni saba za kwenye mkataba wa awali, kodi ambayo itakuwa ikiongezeka kwa asilimia tatu kila mwaka.

Vile vile kodi ya makasha itakuwa Dola 20 kutoka 13 za kwenye mkataba wa awali, ambayo pia itakuwa ikiongezeka kila mwaka kwa asilimia nne.

Alisema pia wamerekebisha kipengele cha utendaji wa kazi ‘perfomance’ na sasa kila baada ya muda TICTS wanatakiwa kuonyesha utendaji kazi wao ikiwamo upakuaji na upakiaji wa makontena.

“Mkataba huo umeondoa masharti hasi ambayo yalikuwa yanabana masilahi kwa Tanzania, ambapo kwa sasa TICTS watalipa kodi ya mwaka ya dola milioni 14 kutoka dola milioni saba za kwenye mkataba wa awali, kodi ambayo itakuwa ikiongezeka kwa asilimia tatu kila mwaka.

“Vile vile kodi ya makasha itakuwa dola 20 kutoka dola 13 za kwenye mkataba wa awali, ambayo pia itakuwa ikiongezeka kila mwaka kwa asilimia nne,’ ’alisema Profesa Mbarawa.

Kwa upande wake, Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Paramagamba Kabudi, aliyeshuhudia utiwaji huo wa saini, alisema mkataba huo ni miongoni mwa mikataba iliyosaidia kujua kwamba kuna umuhimu wa kupitiwa kwa mikataba mingi ambayo imeonekana kutokuwa na manufaa kwa nchi.

 MALALAMIKO DHIDI YA TICTS

TICTS ilikuwa ikituhumiwa kuhusika na upotevu wa mizigo ya wateja na makontena yakiwa yamefunguliwa na kuibiwa baadhi ya mali na mizigo bandarini.
Mara kwa mara Chama cha Wafanyakazi wa Shughuli za Meli na Bandari (DOWUTA), kilikuwa kikiitupia lawama kampuni hiyo kwa kwenda kinyume.

Madai mengine ni kulalamikiwa na baadhi ya watendaji kuinyonya Serikali jambo ambalo tayari limerekebishwa katika mkataba huo.

Pia kucheleweshwa kwa mizigo ya wateja kupakua na kupakia jambo ambalo lilikuwa likipigiwa kelele.

Yote yalifanyika baada ya kamati kuundwa na kufanya uchunguzi wake kwa takribani miezi zaidi ya sita na kutoa majibu ambayo yamefanyiwa kazi kwa kubadili baadi ya vipengele vya mikataba.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles