23.3 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Mkapa na siri ya mafanikio SAUT

Clara Matimo

JULAI 2, mwaka huu,  Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino Tanzania (SAUT) kilitimiza miaka 20 na kufanya  sherehe ya kwenda jubilei ya miaka 25, iliyozinduliwa  rasmi na Rais mstaafu wa Benjamin  Mkapa.

SAUT ilianzishwa  rasmi mwaka 1998, ikiwa ni zao la iliyokuwa  Taasisi ya Elimu ya Sayansi ya Jamii (NSTI), iliyoanza kutoa huduma  mwaka 1960 na wamisionari wa Kanisa Katoliki ambao kwa sasa wanajulikana kama wamisionari wa Afrika wakiongozwa na  Askofu,  Joseph Blomjous wa  Jimbo la Mwanza ambalo  sasa ni  Jimbo Kuu la Mwanza.

NSTI ililenga kutoa mafunzo ya kitaaluma na kitaalamu, ikiwemo  maadili ya elimu ya uraia na kijamii kwa wazawa bila kujali rangi au imani katika nyanja kuu ya usimamizi na utawala pamoja na taaluma ya uandishi wa habari, uhasibu , ugavi na utawala katika masuala ya afya.

Askofu Blomjous alipostaafu mwaka 1964, aliikabidhi NSTI kwa Askofu Renatus Butibubage aliyeiongoza hadi mwaka 1975 na kuikabidhi  kwa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania(TEC) hadi sasa wanaiongoza SAUT

SAUT ilianzishwa ili kukumbatia maadili ya ujumbe wa injili ulivyokuja  katika ulimwengu kupitia neno la Mungu na kwa njia ya mapokeo ya Kanisa Katoliki.

Makamu Mkuu wa SAUT,  Profesa Costa Ricky Mahalu, anasema chuo hicho kimepata  mafanikio mengi  tangu kianzishwe, ikiwamo kuongeza udahili wa wanafunzi kutoka 204 hadi 11,400 kwa mwaka wa masomo 2018/19, huku akibainisha kwamba udahili uliweza kupanda zaidi mwaka 2012/13 na kufikia wanafunzi 13,121, pia wameongeza vitivo vingine vinne kutoka kimoja cha sayansi ya jamii na mawasiliano ya umma ambavyo ni ualimu, sheria,  uhandisi.

Kwa mujibu wa Profesa Mahalu, Rais mstaafu Mkapa ni mtu muhimu katika maendeleo ya chuo hicho  na vyuo vikuu vingine binafsi kwa sababu  ndiye kiongozi wa kwanza akiwa rais aliyeanza kutoa mikopo mwaka 2005  kwa wanafunzi wa elimu ya juu.

Anasema uamuzi huo, ulitokana na mahafali ya kwanza ya chuo hicho yaliyofanyika chuoni hapo mwaka 2001, yeye akia bado rais, wakati huo Makamu Mkuu wa SAUT Dk. Padri Deogratius Rweyongeza, aliiomba Serikali kukisaidia chuo hicho mambo mbalimbali  ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya kutoka Mwanza  kuingia chuoni hapo.

Dk. Padri Rweyongeza, aliiomba pia Serikali  kubadili sera ya mikopo kwa elimu ya juu ili Serikali ianze kuwapa mikopo na wanafunzi wa vyuo vikuu binafsi kwani wakati huo, Serikali ilikuwa inawapatia pesa za masomo ya elimu ya juu wale tu waliokuwa wakisoma vyuo vikuu vya Serikali.

 Anasema maombi hayo yote yalikubaliwa na Rais  Mkapa hivyo mwaka 2002 ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kuanzia Nyegezi Kona mpaka SAUT ulianza na barabara ilizinduliwa mwaka 2004.

Naye Mratibu wa Habari  Kamati ya sherehe za uzinduzi wa miaka 25  ya chuo hicho, Padri Titus Ngapemba, anasema anaamini kuongezeka kwa idadi ya wanafunzi chuoni hapo imetokana na uamuzi mzuri alioufanya Mkapa alipokuwa madarakani kwa kuonyesha upendo kwa wahitaji wote katika sekta ya elimu.

Mkapa anakumbukwa na Watanzania wote  wanaopenda kuona Serikali inawekeza kwenye elimu kwa kuwa muasisi wa utoaji wa mikopo ya elimu ya juu kwa wanafunzi wa vyuo vikuu vyote, vikiwamo,ikiwamo vya binafsi naamini lengo lake lilikuwa ni kuhakikisha watanzania wengi wanapata elimu ya juu.

Hiyo ndiyo siri ambayo SAUT, hawatamsahau mzee Mkapa katika utendaji wao maana maamuzi yake ya kuwa muasisi wa kutoa mikopo kwa wanafunzi wote yalisaidia kutimiza maono ya kanisa katoliki na chuo kwa ujumla ambayo ni maendeleo ya mtu na heshima kwa utu wa binadamu wote.

Hakika Mkapa,ni kiongozi na baba bora maana mzazi anayetimiza wajibu wake siku zote hapendi kuona watoto wake wanakosa mahitaji muhimu ikiwemo marazi, chakula, matibabu na elimu bora ukweli ni kwamba yote haya waliopata mikopo waliyapata kupitia uamuzi wko uliyoyafanya mwaka 2005, Mungu azidi kukupa maisha marefu yenye furaha tele.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles