22.2 C
Dar es Salaam
Friday, August 12, 2022

Mkapa: Majaji, mahakama wawe uhuru

ANDREW MSECHU-DAR ES SALAAM

RAIS mstaafu Benjaman Mkapa,  amesema mahakama ni mhimili muhimu unaotakiwa kuwa huru ili kutenda haki bila kuingiliwa.

Mkapa anatoa kauli hiyo katika simulizi ya kitabu chake cha My Life, My Purpose (Maisha Yangu, Kusudio Langu) alichokizundua hivi karibunu wakati wa  siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake, Novemba 12, mwkaa huu.

Anasema anaamini katika uhuru wa mahakama na kwamba lazima viongozi wawajibike kuhakikisha inakuwa na uhuru wake wa kutosha.

Anasema katika kuheshimu mamlaka ya kisheria, anaamini kabisa linahitaji kuonesha nia ya dhati ya kuipa mahakama uhuru wake inaoustahili kama muhimili kamili, ili kuiwezehsa kujisimamia.

Anasema suala la mamlaka ya uteuzi kwa watumishi uteuzi ni moja, lakini baada ya uteuzi hasa wa majaji kiongozi anayewateua anatakiwa awaachie uhuru wao wa kutosha, na wajisimamie wenyewe, bila kuingiza nguvu au mamlaka ya kisiasa.

“Hili pia nilijifunza kwa Mwalimu (Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere), ambaye alikuwa na maoni makini sana na alipata heshina sana katika hili. Pale ilipoonekana kuna pengo kwenye mfumo wa kimahakama alikuwa akisistiza wanatakiwa watumie utaratibu wao na kuangalia namna ya kuwajibishana,” anasema.

Anasema kwa kawaida majaji ni watu ambao wanatakiwa wawe wameelimika vya kutosha na kuijua vyema sheria, kanuni na taratibu za kisheria, hayo ndiyo maeneo yao ambayo wanatakiwa kuyasimamia ili kujihakikishia uhuru wao.

Anasema uhuru huo ndio msingi wa uwajibikaji wao, katika kuhakikisha wanatoa haki kwa kufuata misingi ya sheria na taratibu, bila uonevu au kukandamiza upande mmoja.

Uzito ofisi ya Rais

Mkapa anasema wakati mwingine ambao ofisi inakuwa nzito ni pale unapokutana na suala linalokulazimisha kutoa msamaha kwa kwa mtu ambaye amehukumiwa kifo kwa kosa la mauaji au la uasi, chini ya mhimili huo huo wa mahakama.

Anasema uamuzi wa Bodi ya Parole huwa unabaki kuwa kama ushauri tu kwa Rais na uamuzi wa mwisho hubaki mikononi mwa rais na kwa kuwa hio ni suala la maisha na kifo, lilimpa taabu sna ana wakati mwisngine hakuweza hata kula chakula, hasa alipoona anatakiwa kutia saini kutekelezwa kwa adhabu.

“Katika miaka 10 ya utawala wangu, nilitoa misamaha, suala ambalo kuna wengine hasakulifurahia.ta walionitangulia hawakuwahi kusaini adhabu ya kifo, ambapo kwa mara ya mwisho ilitekelezwa mwaka 1994. Nakumbuka nilifuta adhabu 100 za kifo na kuzifanya kuwa adhabu za kifungo cha maisha mwaka 2003,” anasema.

Anasema ni wazi  rais ana mamlaka makubwa sana japokuwa si kama miaka ya mwanzo baada ya Uhuru, ambapo alikuwa na uwezo wa kumweka mtu kizuizini kwa muda wowote anaopenda.

Anasema kwa nyakati hizi, atatakiwa kumpeleka mahakamani na kueleza kwamba kwa nini unaamua kumshikilia mtu, sababu hiyo pia itachunguzwa na mahakama ambayo itaamua iwapo hatyua hiyo ni sahihi au la.

Mkapa anaeleza anakumbuka, yeye aliunga mkono na kusimamia kupitishwa kwa utaratibu huo wa kupunguza mamalaka hiyo ya kumweka mtu kizuizini bila maelezo.

Anasema anaamini na kuthamini mgawanyo wa madaraka na mamlaka kupitia mihimili iliyopo, yaani Bunge, Serikali na Mahakama, akisisitiza kuwa hilo ni suala la muhimu sana hasa kwa nchi hizi zinazoendelea.

“Nakumbuka, hili lilikuwa moja ya mambo niliyoyazungumza wakati tulipokuwa tukitoa maoni kuhusu Katiba mpya, mwaka 2015. Lazima kuwe na muundo rasmi unaotenganisha kwa uwazi madaraka ya Rais, au kuweka utararatibu wa kumpa rais muda wa kukaa na kutafakari.

“Nadhani hapa ndipo kunapoonekana kuwa na umuhimu wa kuwapo kamati ya kibunge inayotoa nafasikwa wale wenye uzoeefu kupitia kwanza baadhi ya mambo kabla rais hajatia saini. Si lazima iwe na wataalamu walioajiriwa, inaweza kuwa kama timu ya washauri ambao wanatoa tahadhari kuhusu matokeo hasi ya miswada inayopitishwa kabla ya kusainiwa na Rais.

“Kwa namna fulani hii inaweza kumwepushia Rais lawama kwa kuwa hatakuwa tayari kusaini miswada isiyokuw ana tija na kuwa sheria,” anasema.

Utoaji wa uamuzi

Mkapa anasema wakati wa utawala wake, alijitahidi kuwa wazi na kushirikiana na mawaziri wake kwa karibu kabisa.

Anasema alipoingia madarakani, kwa mtu ambaye hakumjua vyema awali alitambua kuwa hakuwa mtu mwoga, hakufanya lolote kwa woga na kwamba kiongozi lazima awe mtu wa kuwapa watu moyo wakati mwingine.

Anasema ilipotokea tatizo katika wizara, aliwasiliana na waziri mkuu, kisha waziri husika na mara nyingi alipenda kumshirikisha Mwanasheria Mkuu wa Serikaki ambaye alikuwa akitoa mtizamo wa kisheria kuhusu suala husika.

Anasema wakati wote aliwasisitiza mawaziri kujua mipaka yao kimamlaka na ni wakati gani wanatakiwa kutumia mamlaka yao na wakati gani hawahitaji kuyatumia.

“Ninapokaa na kuangalia nyuma sasa, ninabaini kuwa niliwahi kufanya makosa kwa baadhi ya watu waliokuwa wateule wangu, katika mihula yangu miwili ofisini,” anasema.

Anasema alikuwa wazi sana kwa mawaziri wake na alijifunza kutoka kwa Mwalimu Nyerere kuwa mtulivu, msikivu na kutafuta suluhu kwa kadiri ilivyowezekana, lakini zaidi kuweka mazingira bora na shirikishi ya utendaji kazi.

Anasema kwa baadhi yao ambao waliwahi kufanya kazi na Mwalimu, waliwahi kushuhudia akitoa ufumbuzi wa matatizo lakini akiendelea kutoa nafasi ya majadiliano ili kuwapa wengine wasaa wa kuelewa kwa undani kuhusu maamuzi aliyoyatoa.

“Nilijaribu kufuata utaratibu huo wa kushauriana na baraza langu la mawaziri. Niliona ilikuwa vyema kwangu katika utendaji, kwa sababu kwanza wengi tuliokuwa katika umri unaokaribiana, kwa hiyo majadiliano yetu yalikuwa wazi sana.

“Hata hivyo kulikuwa na changamoto hasa kufikia makubaliano na baadhi ya mawaziri wangu na nilikuwa makini sana katika mambo yanayohusu masuala ya kisera, nilikuwa nikifanya juhudi zaidi kujua kwa undani kwa hiyo haikuwa rahisi kwangu kufanya uamuzi usiyo sahihi,” anasema.

Anasema mara nyingine baraza lilikuwa likikosea maamuzi yake na kuwa walikuwa na utamaduni wa kulifanya baraza kuwa mshauri wa rais, walimshauri na hatimaye rais alitoa uamuzi.

“Rais anaweza kupuuza ushauri wowote anaopewa na matokeo yake ni kwamba iwapo kuna waziri aliyeona hakutendewa haki katika hilo, alikuwa huru kujiuzulu, ninashukuru  haikutokea waziri yeyote kujiuzulu kwa sababu hiyo katika utawala wangu,” anasema.

Anasema alitambua yeye ndiye anayebeba majukumu yote na kwamba kuna wakati alilazimika kuwaambia mawaziri wanne wajiuzulu, watatu katika kipindi chake cha kwanza ambao ni Juma Ngasongwa, Profesa Simon Mbilinyi na Kilontsi Mporogonyi, japokuwa badaye alimrejesha Ngasongwa, baada ya uchunguzi kumsafisha.

Anasema katika kipindi chake cha pili, aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara, Iddi Simba alijiuzulu baada ya kuonekana alikuwa akitumia mamlaka yake kuhusisha shughuli za Serikali na masilahi yake binafsi.

Anasema mwingine alikuwa Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais, Hassy Kitine, ambaye alilazimika kujiuzulu baada ya kubainika mkewe alitoa taarifa za uongo kuhusu gharama za matibabu aliyofanyiwa huko Marekani.

Mkapa anasisitiza ni muhimu kiongozi kuwa karibu na watu japoikuwa inahitaji ujanja ili kukua wakweli na wasio wema, hasa katika nchi hizi zinazoendelea ambapo ukiwa katribu sana na watu fulani hutumia nafasi hiyo kama njia ya kujinufaisha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,526FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles