24.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 31, 2023

Contact us: [email protected]

Mkapa afunga jalada mgogoro wa Burundi

Na ELIYA MBONEA – ARUSHA


RAIS Mstaafu Benjamin Mkapa ambaye ni msuluhishi wa mgogoro wa siasa Burundi, anatarajiwa kuwasilisha ripoti maalumu iliyotokana na mapendekezo ya pande mbili zinazovutana kwa Msuluhishi Mkuu, Rais Yoweri Museven wa Uganda.

Hatua hiyo ni baada ya kumalizika   mazungumzo yaliyofanyika kwa siku tano mkoani Arusha na kutolewa mapendekezo ya kumaliza mgogoro huo.

Hata hivyo upande wa Serikali ya Burundi ulisusa kushiriki moja kwa moja licha ya kuwasilisha mapendekezo yake kwa msuluhishi.

Akizungumza baada ya kumalizika mazungumzo yaliyofanyika katika Hoteli ya Ngurdoto wilayani Arumeru mkoani Arusha, Mshauri Mkuu wa ofisi ya msuluhishi wa mgogoro huo, Balozi David Kapya, alisema ripoti hiyo itawasilishwa mapema kwa Rais Museven.

Balozi Kapya alisema mazungumzo hayo ya siku tano yalishirikisha marais wastaafu wa Burundi, Makamu wa Rais, Spika mstaafu na viongozi wa vyama vya siasa kutoka nje na ndani ya Burundi  ambao kwa pamoja walitoa mapendekezo yao ya namna ya kumaliza mgogoro huo.

“Washiriki wanaamini mapendekezo hayo kama yatafanyiwa kazi, mgogoro uliopo nchini humo utakuwa umeisha.

“Mshuluhishi Mzee Mkapa ameshukuru sana kwa viongozi hao kufanya kazi kwa pamoja kama kundi, hawakugawanyika mpaka walipofikia hatua ya kuwasilisha mapendekezo yao na kuja na kitu kimoja, hii ni hatua nzuri kwao,” alisema Balozi Kapya.

Alisema kwa sasa Mkapa ataangalia na kusoma kwa kina mapendekezo  kutoka kwa viongozi hao pamoja na yale yaliyowasilishwa na   Serikali ya Burundi.

“Baada ya kusoma mapendekezo yote atatengeneza taarifa atakayoiwasilishwa kwa Rais Museveni ambaye naye ataiwasilishwa kwa wakuu wa nchi za Afrika Mashariki,” alisema Balozi Kapya.

Aliwataka kuangalia Mkakati wa Entebe wa 2018 uliopendekezwa na vyama vya upinzani vya ndani na nje ya nchi hiyo na mapendekezo yaliyotolewa na vyama vya jamii, wanawake, vijana, vyombo vya habari na makundi ya dini katika mkutano wao uliofanyika Oktoba 20 hadi 22, mwaka 2018.

Alisema aliwataka kuangalia taarifa za mikakati hiyo  kuiweka katika misingi ya uchaguzi unaotarajiwa kufanyika 2020.

“Mapendekezo mliyotoa katika kikao kilichomalizika jana, yamekuwa mazuri katika kutatua mgogoro huu na hakika mmeonyesha umoja bila kujali itikadi za vyama vyenu.

“Kama nilivyowaeleza awali wakati nikifungua mkutano huu, huu utakuwa mkutano wangu wa mwisho wa mazungumzio ya usuluhishi wa mgogoro huu.

“Kwa maana hiyo nitawasilisha mapendekezo mliyotoa kuzingatia mikakati ya Kayanza 2013 na Entebbe 2018, pamoja na ripoti kamili ya mchakato wa mazungumzo haya kwa msuluhisi mkuu (Rais Museveni) ambaye atawasilisha kwa Mkutano Mkuu wa Viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki,” alisema.

Mwenyekiti wa Chama cha Umoja wa Amani kwa ajili ya Maendeleo (UPD), Chauvieneau Mugwengezo, alisema wanaunga mkono kumalizika kwa mazungumzo hayo.

Alisema kama wapinzani, mazungumzo hayo yalikuwa na fursa kwa kukaa pamoja lakini alishangaa kuona upande wa Serikali ya Burundi hawakuweza kuhudhuria

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,207FollowersFollow
567,000SubscribersSubscribe

Latest Articles