28.4 C
Dar es Salaam
Thursday, February 22, 2024

Contact us: [email protected]

Mkanda waongeza mzuka pambano la ‘Queen of the Ring’

Na Winfrida Mtoi, Dar es salaam

Homa ya pambano la  ngumi la ubingwa wa dunia lililopewa jina la ‘Queen of the Ring’, linalowakutanisha mabondia wa kike, Zulfa Macho na Halima Vunjabei, imezidi kupanda baada ya kila bondia kutamba kuibuka malkia wa taji hilo.

Mzuka wa mabondia hao umepanda baada ya  waandaaji wa mchezo huo, leo kutambulisha mkanda unaogombaniwa mbele ya waandishi wa habari.

Pambano hilo la raundi 10, linatarajia kufanyika  Jumapili hii Aprili 11, 2021 kwenye Ukumbi wa Ubungo Plaza, Dar es salaam huku kukiwa na mapambano kibao ya utangulizi ya wanaume na wanawake.

Wakizungumza  na waandishi wa habari katika Gym ya City Mall, Dar es Salaam,  mabondia hao, wametamba kuwa hakuna maneno mengi zaidi ya kutwangana ulingoni.

“Pambano hili halijawahi kutokea Tanzania, naomba uzima nifike siku ya mchezo, napenda kuwaahidi  Watanzania na mashabiki wangu kuwa mkanda huu utabaki kwa Halima Vunjabei kutokana na mazoezi niliyofanya,” amesema bondia Halima.

Kwa upande wake Zulfa, amesema kutokana na maandalizi yake ya miezi kadhaa, yanatosha kabisha kuondoka na taji hilo na anaamini watu wake wanahitaji ushindi.

Mratibu wa pambano hilo, Kapteni Selemani, Semunyu, amesema maandalizi yanaendelea vizuri  na mchezo huo utakuwa na mvuto mkubwa kutokana na aina ya mabondia wanaopigana.

“Peaktime tumeamua kulifanya pambano hili la kipekee na tumeweka kiingilio  cha kuanzia h. 10,000 ili kila mmoja ajitokeze kuja kuwasapoti wanawake hawa wenye vipaji vya juu,” amesema  Kapteni Semunyu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles