26.9 C
Dar es Salaam
Friday, December 9, 2022

Contact us: [email protected]

Mkakati wa kukifuta chama cha Bobi Wine wapelekwa mahakamani

 KAMPALA, UGANDA

MWANASIASA wa upinzani nchini Uganda anayemtikisa Rais Yoweri Museveni amejikuta akipigania mchakato wa kuwa kwenye karatasi ya kura, baada ya mshirika wake kukanusha mahakani kwamba alimpa uongozi wa chama cha NUP.

Sakata ya kesi ya kupinga uhalali wa chama cha kisiasa cha Bobi Wineilianza wiki iliyopita pale mshirika wa Bobi Wine, Moses Kibalama ambaye alionekana kwenye kanda ya video iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii akidai kuwa Bobi hakutimiza ahadi yake ya kumlipa Dola milioni 5 za Kimarekani pale alipokubali kumwachia chama chake cha kisiasa cha NURP.

Awali, Kibalama aliwasilisha nyaraka mahakamani akimtetea Bobi Wine kuwa kiongozi wa chama hicho wakati wenzake alioanzisha chama nao kuwasilisha kesi wakidai kuwa hawamtambui Bobi Wine kuwa kiongozi wa chama chao.

Wiki iliyopita, Kyagulanyi alifika mahakamani hapo, hata hivyo Jaji Musa Ssekaana aliahirisha kesi, na kuwapa samansi Moses Nkonge Kibalama na Paul Ssimbwa Kagombe kufika mahakamani hapo Septemba 25 kwa ajili ya kuhojiwa kuhusu masuala ya chama hicho.

 Kibalama alifika mahakamani Ijumaa pamoja na Ssimbwa wakiwa chini ya ulinzi wa askari wa kikosi cha ulinzi wa rais Museveni. 

Katika mahojiano na mawakili wa Bobi Wine, wawili hao walithibitisha kuwa walimkabidhi Bobi Wine chama chao, hali iliyomuacha jaji katika dhima kubwa ya kuamua kesi hiyo tarehe 16 mwezi Oktoba.

Bobi Wine aliilezea kesi hiyo kuwa hila ya Rais Museveni kuhakikisha kuwa hafanikiwi kushiriki kwenye kinyang’anyiro cha urais. Katikaujumbe aliouweka kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii, Bobi Wine alisema Kibalama anashurutishwa na utawala. “Rais wetu wa zamani, Nkonge Kibalama amethibitisha mahakamani kwamba amekuwa chini ya kizuwizi kwa wiki mbili. Ameiomba mahakama imsaidie kupata uhuru wake. Anasema aliitwa na Jenerali Muhoozi, mkuu wa majeshi aliemhoji kuhusu mabadiliko ya uongozi wa chama!” aliandika Bobi Wine.

Kwa sasa chama cha NUP kimeshiriki katika uchaguzi wa vijana na wanawake na wagombea wake wameshinda baadhi ya viti. 

Ikiwa mahakama itafutilia mbali chama hicho hata tume ya uchaguzi itakuwa mashakani kuandaa uchaguzi mwingine kwa nafasi hizo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,735FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles