24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Mkakati mpya Muhimbili

Mwandishi Wetu, Dar na Dodoma

HOSPITALI  ya Taifa Muhimbili (MNH), imefunga mashine tatu za kusafisha damu kwa wagonjwa wenye matatizo ya figo ambao pia wana maambukizi ya virusi vya corona(Covid-19) ambao wanapatiwa huduma  katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa  Amana. 

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma, Aminieli Aligaesha alisema kuwa mashine hizo zina thamani ya  zenye Sh milioni 210,huku wakitarajia  kufunga mashine moja ya kusaidia mgonjwa kupumua (ventilator) yenye thamani ya Sh milioni 56.

 “Tayari wagonjwa wanaohitaji huduma ya kusafishwa damu wameanza kuhudumiwa na wafanyakazi wa Muhimbili  waliopo Hospitali ya Amana tangu Ijumaa, dawa na vitendanishi vya kutoa huduma ya kusafisha figo kwa sasa vinagharimiwa na Hospitali ya Muhimbili,”alibainisha Aligaesha.

Alisema  sambamba na hilo, Hospitali imefunga mtambo wa kuchuja maji (Portable RO) wenye thamani ya Sh milioni 28 na mtandao wenye miundombinu ya kusafirisha maji ili kuwezesha mashine hizo kufanya kazi ya kusafisha damu ambao  umegharimu Sh milioni  12 . 

“Kutokanana hilo, Muhimbili  itapokea madaktari na wauguzi kutoka Hospitali ya Rufaa ya Amana kuanzia Aprili 28, mwaka huu ili kujengewa uwezo kwenye kitengo cha kusafisha damu pamoja na vyumba vya wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu (ICUs) aina tano tofauti,”alisema.

Alisema  hospitali hiyo,  ilipokea wagonjwa 93 kutoka Amana, wakiwemo watoto wachanga 30 wa chini ya mwezi mmoja wakiwa na mama zao.

” Watoto wanne wa chini ya miaka mitano, kina mama wajawazito 36, wagonjwa wa upasuaji 10 na wagonjwa 13 wenye magonjwa ya ndani (internal medicine).

 “Muhimbili imekua bega kwa bega na uongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam kwenye maandalizi ya kupokea wagonjwa waliopata maambukizi ya corona kutoka hospitali Rufaa ya Amana, ikiwa ni hatua ya kuunga mkono juhudi za Serikali za kuhakikisha wagonjwa waliolazwa wanapata huduma,”alisema. 

Alitoa  rai kwa wananchi kuendelea kuchukua tahadhari ili kujinga na kuwakinga watu wengine kulingana na maelekezo yanayotolewa na Serikali.

DODOMA

Katika hatua nyingine, Askofu wa Kanisa la Maombezi (EHC), Dk.Eliah Mauza ameiomba  Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na watoto kuhakikisha dawa za tiba mbadala, zitakazotumika zinathibitishwa  na mamlaka husika ili kundoa wimbi linaloibuka hivi sasa la kila mtu kudai ana dawa ya kutibu ugonjwa huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles