Mji mkuu wa Angola, Luanda, umechukua nafasi ya kwanza kama mji ghali zaidi duniani kwa wataalamu na kuusukuma mji wa Hong Kong hadi nafasi ya pili.
Hii imetokana na takwimu za gharama ya kuishi kutoka na utafiti ulifanywa na shirika la Mercer
Miji ya Tokyo, Zurich na Singapore pia nayo inachukua nafasi tano za kwanza.
Mji wa London ulishuka hadi nafasi ya 30 hasa kutokana na kushuka kwa thamani ya pauni.
Utafiti huo wa kila mwaka huangazia masuala kadha kando na gharama ya kukodi nyumba.
Utafiti huo huangazia gharama ya vitu 200 kwa kila mji, ikiwemo nyumba, usafiri, mavazi, chakula na burudani.