24.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

MJASIRIAMALI KUUNDA KOLONI LAKE SAYARI YA MARS

JOSEPH HIZA NA MTANDAO


MWANZILISHI wa Kampuni za Tesla na SpaceX, Elon Musk hivi karibuni ametangaza kuwa mpango wake wa kuunda koloni katika Sayari ya Mirihi (Mars) imeiva akianza kupeleka chombo cha anga za juu mapema mwaka ujao.

Mradi huo unaofadhiliwa kibinafsi ulitangazwa Septemba 2017, ukilenga kusafirisha mizigo kwenda sayari hiyo nyekundu ifikapo 2022.

Hata hivyo, lengo kuu la kampuni ya anga za juu ya SpaceX ni kuunda koloni la binadamu katika sayari hiyo litakalokaliwa na watu zaidi ya milioni moja.

Tiketi ya kusafiri hadi kwenye sayari hiyo, inakadiriwa kugharimu takriban dola 200,000 sawa na Sh milioni 430.

Musk, alitangaza mpango huo katika kongamano la kimataifa la wataalamu wa anga za juu (IAC) mjini Guadalajara, Mexico.

Mpango wake, unajumuisha mfumo wa usafiri ambao utaweza kusafirisha watu 100 hadi Mars, safari yote ikichukua siku 80.

Baadaye, safari hiyo inatarajiwa kuchukua siku 30 pekee.

Musk amesema ili kufanikisha hilo kila mtu atatakiwa kutoa Sh milioni 430.

Amezungumzia mpango wa kuunda koloni la watu milioni moja ambao wataweza kujitosheleza na kusema mpango huo utachukua miaka 10 hivi kukamilika.

Ili kufikisha watu milioni moja, Musk anasema: “Ninataka watu watazame kwamba ni jambo linalowezekana, jambo tunaloweza kutimiza katika uhai wetu… na kwamba yeyote anaweza kwenda huko akitaka.”

Chini ya mpango wa SpaceX, safari ya kwanza ya kupeleka watu sayari hiyo itafanyika 2022.

Chombo cha kwanza kupeleka watu Mars, Musk anataka kukiita The Heart of Gold, jina linalotokana na chombo kinachozungumziwa katika kitabu cha Douglas Adams The Hitchhiker’s Guide to the Galaxy.

Kitarushwa kutoka Kituo cha Anga za Juu cha Nasa cha Keneddy, sehemu 39, ambayo ndiyo iliyotumiwa kurusha roketi na vyombo vya anga za juu chini ya mpango wa Apollo.

Chombo cha kwanza cha kusafirisha watu kitafanyiwa majaribio katika kipindi cha miaka minne ijayo.

Mwishoni mwa wiki, Musk alitangaza kwamba majaribio ya kwanza ya roketi kwa jina Raptor ambayo itatumiwa kurusha chombo hicho pamoja na kifaa cha kuiweka kwenye mzunguko anga za juu (booster) yalifanyika.

Tangi la mafuta ya kifaa hicho limeundwa na kufanyiwa majaribio na Musk, ambaye alionesha picha ya tangi hilo na wafanyakazi.

Mfumo wa kifaa hicho cha kuweka chombo cha anga za juu kwenye mzunguko wa sayari, pamoja na chombo chenyewe, kwa pamoja unaitwa Mfumo wa Usafiri wa Sayari hadi Nyingine (ITC).

Mitambo hiyo miwili kwa pamoja ina urefu wa mita 122, na inazidi mfumo wa Saturn V wa Apollo ambao ulitumiwa kwenda mwezini.

Mjasiriamali huyo anapanga kwamba wakati wa safari hiyo ya siku 80, watu wataishi kwa pamoja na kutazama filamu, kuhudhuria mihadhara na kucheza michezo isiyoathiriwa wa mvutano wa sayari.

Mpango wote utafadhiliwa kwa faida kutoka kwa SpaceX.

Musk anatazama mpango huo wa kupeleka watu Mars kuwa na ushirikiano mkubwa wa umma na sekta binafsi na anasema hivyo ndivyo Marekani ilivyoanzishwa.

Vyombo vya anga za juu vitatumwa kila baada ya miaka miwili Mars inapokuwa imekaribia dunia. Umbali kati ya sayari hizo mbili utakuwa kilomita 57.6 milioni mwaka huu 2018.

Sayari hizo zinapokuwa mbali, huwa umbali kati yake ni kilomita 400 milioni.

Miaka ya karibuni, umbali huo umepungua kufikia kilomita 100 milioni pekee.

Musk anasema chini ya mpango wake, kunawezekana kuwa na vyombo 1,000 vikisafiri angani.

Gharama ya kusafiri baadaye inaweza kushuka hadi kati ya dola 100,000 na dola 140,000.

Anasema: “Mtu akitaka kurejea duniani, ataweza kufanya hivyo bila malipo.” Je, ndoto hiyo itatimia? tusubiri!

 

 

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles