32.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 23, 2024

Contact us: [email protected]

‘Mjadala uendelezaji bandari ujikite kwenye hoja’

Na Nora Damian, Mtanzania Digital

Mwenyekiti wa Taasisi ya Kiislamu ya Imamu Bukhary, Sheikh Khalifa Khamis, ameshauri mjadala kuhusu uendelezaji wa bandari ujikite kwa kujenga hoja na kutoa mapendekezo kwa nia ya kupata suluhisho lenye manufaa kwa Watanzania.

Akizungumza na waandishi wa habari Juni 22,2023 amesema baadhi ya watu wamekuwa wakijadili suala hilo kwa kutumia maneno yasiyo na staha kwa nia ya kueneza chuki miongoni mwa Watanzania.

Amesema Rais Samia ana lengo la kuboresha ufanisi wa shughuli za bandari uwe na tija ili Serikali ipate fedha zaidi kwa manufaa ya Watanzania wote.

“Kila Mtanzania ana haki ya kujadili ama kutoa maoni yake juu ya taasisi yoyote ya umma, lakini jambo hili lazima lifanyike kwa kujenga hoja, kutoa mapendekezo kwa nia ya kupata suluhisho lenye manufaa kwa Watanzania.

“Wanaopinga wawe na hoja za msingi, Watanzania wajiepushe na mijadala ya ubaguzi na udini kwa sababu sisi sote ni wamoja,” amesema Sheikh Khamis.

Amesema pia baadhi ya vitengo vya bandari vimekuwa vikiendeshwa kwa ubia baina ya Mamlaka ya Bandari na kampuni zisizo za Serikali hivyo kinachotaka kufanywa sasa si jambo jipya.

Mwenyekiti huyo ameshauri wananchi waeleweshwe kuhusu manufaa ya uwekezaji huo na uwezo wa kampuni husika na maoni yao yasikilizwe.

Juni 10, 2023 Bunge lilipitisha azimio kuhusu makubaliano ya ushirikiano wa uendelezaji wa bandari kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Dubai Port World (DPW) inayomilikiwa na Serikali ya Dubai.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles