Mizigo kuanza kusafirishwa kwa reli

Profesa Makame Mbarawa,Na ELIUD NGONDO, SONGWE

WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, amesema Serikali ina mpango wa kuhakikisha mizigo inasafirishwa kwa njia ya reli badala ya barabara.

Akizungumza jana katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mbarawa alisema ili kuondokana na uharibifu wa barabara, lazima mizigo isafirishwe kwa reli kwa kuwa magari yanaharibu barabara.

“Magari makubwa yanayobeba mizigo na kuipeleka nchi za Kusini mwa Afrika, yanaharibu barabara na sasa umefika wakati wa kuchukua hatua.

Kwa upande wake, Meneja wa Uwanja wa Ndege wa Songwe, Hamisi Amiri, alisema mkandarasi wa kwanza ambaye ni Kampuni ya Kundasighn, alishindwa kukamilisha ujenzi huo na kusababisha mradi usikamilike kwa wakati.

“Baada ya kampuni hiyo kuondoka, sasa tuna Kampuni ya Shamphrey ambayo imeanza ujenzi ingawa haijawahi kulipwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here