27.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Mitaa 159 kushiriki uchaguzi Serikali za Mitaa

CHRISTINA GAULUHANGA-DAR ES SALAAM

HALMASHAURI ya Manispaa ya Ilala, Dar es Salaam ina  mitaa 159  ndani ya kata 36  ambayo itashiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa, unaotarajiwa kufanyika Novemba  24, mwaka huu.

Akitangaza mitaa hiyo na mipaka kwa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala ,Msimamizi Mkuu wa Uchaguzi, Elzabeth Thomas amesema   mamlaka  hayo amepewa chini ya kanuni ya tano ya uchaguzi wa mwenyekiti wa Serikali ya mtaa na wajumbe wa kamati za mtaa katika gazeti la Serikali Aprili, mwaka huu.

“Orodha ya mitaa ilitangazwa katika gazeti  la Serikali Julai, mwaka huu majina ya mipaka ya mitaa kwa ajili ya uchaguzi huu ambapo kuna kata 36,mitaa yote 159  itasimamisha wagombea,”alisema Thomas

Alitaja baadhi ya mitaa kuwa ni Kata ya Upanga Mashariki, Kitonga , Kibasila, Upanga Magharibi Mfaume, Fire, Charambe.

Nyingine ni kata ya Kivukoni, Seaview,Kivukoni, Jangwani ,Mtambani A, Mtambani B, Mnazi Mmoja na Ukombozi.

Mingine ni Kariakoo Mashariki, Kaskazini, Magharibi, Kisutu , Gerezani , Gerezani Magharibi na Mashariki, Kata ya Mchafukoge, Mchafukoge na Kitumbini.

Alisema mitaa mingine ni kata ya Vingunguti,mtaa wa Kombo, Mtakuja, Miembeni, Butiama, Mtambani Majengo, Kata ya Tabata ,Tenge, Mandela,Tabata,Kisiwani, Msimbazi Magharibi ,Mtambani, Matumbi na Kisiwani.

Aliwataka wananchi kupita katika ofisi za maofisa watendaji wa kata zao kwa lengo la kupata elimu na kufahamu eneo la kituo watakachojiandikisha ili kupiga kura.

“Viongozi bora wa serikali za Mitaa ni chachu ya maendeleo ni haki na wajibu wako kuchagua kiongozi bora kwa maendeleo ya Taifa, “alisema Elizabeth.

Aliwaimiza wananchi kushiriki uchaguzi wa Serikali  za Mitaa 2019,demokrasia huzaa maendeleo endelevu amani na mshikamano.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles