22.2 C
Dar es Salaam
Monday, October 18, 2021

MISUNGWI YATENGA MILIONI 240/- KUJENGA SEKONDARI

  Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Eliud Mwaiteleke

 

Na PETER FABIAN,

HALMASHAURI ya Wilaya ya Misungwi, imetenga Sh milioni 240 kwa ajili ya kujenga sekondari za kidatu cha sita kwa tarafa nne za wilaya hiyo ili kupanua wigo wake wa elimu.

  Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Eliud Mwaiteleke, alisema hatua hiyo inatokana na mkakati wake wa kuboresha miundombinu ya baadhi ya shule zake za sekondari   kuzipandisha hadhi ziweze kuwa na kidato cha tano na sita.  

Mwaiteleke alisema  halmashauri imetenga   Sh milioni 240 ambako kila sekondari imetengewa Sh milioni 80 kwa ajili ya kujenga madarasa mawili kila moja likigharimu Sh milioni 20 huku  wananchi wakitakiwa kuchangia fedha na nguvu kazi zao wakati wa ujenzi kwa asilimia 20.

“Tumeadhimia katika vikao vyetu vya maendeleo ya wilaya kuwa lazima tuhakikishe tunapandisha hadhi sekondari moja iliyopo katika kila tarafa ili kuwa na high school, lengo ni wanafunzi wapate elimu hiyo ndani ya wilaya yetu badala ya kuitafuta wilaya jirani,”alisema.

Mkurugenzi huyo alizitaja shule za sekondari na tarafa zake kwenye mabano kuwa ni Paul Bomani (Usagara), Mbalika (Mbalika), Misasi (Inonelwa) huku sekondari ya Misungwi (Misungwi) tayari ikiwa imekisha kuanza na kuwa na wahitimu wa kidato cha sita tangu mwaka jana.

Mwaiteleke alisema pamoja na kutenga bajeti kiasi hicho na kutegemea michango ya wananchi zikiwamo fedha na nguvu kazi lakini pia wamewasilisha ombi la fedha Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)  kusaidia utekelezaji wa malengo hayo kwa mwaka huu.

“Kama halmashauri na wilaya katika kufanikisha malengo ya ujenzi huo pia tumeandaa kuwa na harambee   Juni ambayo tunatarajia wadau mbalimbali wa maendeleo, marafiki na wananchi kuchanga fedha.

“Lengo la fedha hizo  ni kufikia malengo ya uboreshaji miundombinu ya elimu ikiweamo kuongeza vyumba vya madarasa, matundu ya vyoo, vyumba vya maabara, thamani na nyumba za walimu,” alisema.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
162,220FollowersFollow
521,000SubscribersSubscribe

Latest Articles